Kamishna wa Huduma za Urekebishaji wa Jeshi la Magereza, Deonice Chamulesile akiwaongoza Mamia ya Waombolezaji katika kutoa heshima za mwisho kwa Marehemu Sajini wa Magereza, Peter Shelukindo aliyefariki kwa ajali ya gari Aprili 22, 2014 majira ya saa Saba mchana wakati akisindikiza Mahabusu kutoka Mahakama ya Mwanzo Kimanzichana Wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani. Katika ajali hiyo pia walikufa Mahabusu wanne waliokuwa wanatoka kusikiliza kesi zao.
 Baadhi ya Askari wa Jeshi la Magereza wakiaga mwili wa Marehemu Sajini wa Magereza, Peter Shelukindo katika Kambi ya Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam leo Aprili 24, 2014.
 Mke wa Marehemuakisaidiwa na mmoja wa Waombolezaji kumuaga Mme wake aliyekufa kwa ajali ya gari.

Baadhi ya Waombolezaji walijitokeza kuuaga mwili wa Marehemu Sajini wa Magereza Peter Shelukindo aliyekufa kwa ajali ya gari Wilayani Mkuranga(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...