Na Andrew Chale

MBUNIFU mkongwe wa mitindo nchini, Asia Idarous Khamsin anatarajiwa kufanya onyesho kubwa la mavazi ya ubunifu katika maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, litakalofanyika Abuja, Nigeria,  usiku wa Aprili 25, 2014.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Abuja, Nigeria,  Asia Idarous ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fabak Fashions, alisema onyesho lililoandaliwa na Umoja wa watanzania waishio nchini Nigeria, ambapo usiku huo wa Aprili 25, watakutana kwa pamoja na kufurahia miaka 50, ya Muungano, utakaoadhimishwa  siku ya April 26.

Alisema onyesho hilo la Miaka 50 ya Muungano, ataonyesho mavazi mbalimbali ya ubunifu ambayo kwa kiasi kikubwa yataitangaza Tanzania na Afrika kwa ujumla, ambapo pia anatarajiwa kukutanisha magwiji wengine wa ubunifu wa nchi hiyo.
"Nashukuru nimefika salama, Nigeria toka juzi na tayari maandalizi yanaendelea vizuri, Usiku wa April 25, majaliwa tunafanya onyesho letu maalum” alisema Asia Idarous kwa njia ya simu.



Asia Idarous alisema kufanya onyesho nchini Nigeria, ni heshima kubwa sana kwake na tukio la kihistoria hasa akiiwakilisha Tanzania katika kutimiza miaka 50 ya Muungano wake tokea hiyo 1964 hadi leo 2014, ambapo ni Muungano pekee barani Afrika na wakuigwa.

“Utanzania wetu ni Muungano wetu,  tuulinde, tuumalishe na kuudumisha  ndani na nje ya mipaka yetu, hakika onyesho hili pia litaendelea kuwa la kuongeza tija ya umoja wetu ikiwemo watanzania waishio nje ya mipaka yao ‘Diaspora’” alisema Asia Idarous.

 Nigeria ni miongoni mwa nchi pekee zenye kudumisha utamaduni wake ukiwemo wa mavazi yenye kuwatambulisha watu wa jamii hiyo, tasnia ya ubunifu na mitindo imekuwa ikipewa kipaumbele hali inayopelekea tija  na hata Taifa hilo kuwa juu kiuchumi.

Aidha, Asia aliwataka watanzania hasa wabunifu wa mitindo na wasanii kubadirika kwa kujikita katika kufanya kazi zenye tija kwa ukuaji wa uchumi kama walivyofanikiwa kwa Wanaigeria.

Asia Idarous ama Mama wa Mitindo, amedumu kwenye fani hiyo kwa muda mrefu huku pia akifanikiwa kufanya maonyesho katika mataifa mbalimbali duniani likiwemo Marekani na kwingineko,  Nchini amekuwa akiandaa maonyesho ya mitindo ikiwemo  la ‘Usiku wa Khanga za Kale’ na lile la ‘Red in Lady’, yanayofanyika kila mwaka nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...