Tubingen,Ujerumani,Ilikuwa usiku  jumamosi  19.Julai 2014 bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni " imefanikiwa tena kuwatia wazimu malefu ya washabiki katika maonyesho makubwa ya International African Festival 2014 mjini Tubingen,Ujerumani. 

Bendi hiyo iliyobatizwa majina mengi ya utani na washabiki wake  imejikuta inaongeza idadi ya maelfu ya washabiki katika maonyesho yake.

Katika hali isiyo ya kawaida usiku wa jumamosi 19 Julai 2014 Ngoma Africa band
imejikuta  ipo ikitingisha jukwaa kwa muziki moto moto ambao mbele ya jukwaa kulikuwa na umati wa washabiki na nyuma ya jukwaa kukiwa na magari maalumu ya Polisi wa kuzuwia ghasia wa kijerumani ambao walikuwa tayari kwa lolote lile!

Maelfu ya washabiki wakiwa wanajirusha bila ya mashaka na muziki wa FFU-ughaibuni aka viumbe wa ajabu Anunnaki Alien ukipenda watoto wa mbwa chini ya uongozi wake mwanamuziki Ebrahim Makunja aka kamanda Ras Makunja.

Wadau mbali mbali walihojiwa katika maonyesho hayo wameitaja bendi hiyo kila kukicha inazidi kujizolea wingi wa umati wa washabiki kutokana na mvuto na umahili wake. Ngoma Africa band inatajwa ndio bendi pekee ughaibuni inayoongoza kuwa na washabiki wa lika,jinsia na mataifa mbali mbali.
Kamanda wa FFU,Ras Makunja akiongoza mashambulizi.
Binti Komando wa FFU Band akifanya yake.
Mashambulizi yakiendelea.
nyomi uwanjani hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2014

    FFU mnatisha, washabiki wenu ni mchanganyiko wa mataifa, sasa wafanyieni mpango wasanii wenzenu wanakuja huko kupiga ktk paty za watanzania tuu

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2014

    sasa nyie ffu mbona mna mtandao mkubwa ,sasa mbona wasanii wenzenu wakijaga huko wanawatumbuiza wabongo tu? je ? mnaweza kuwaunganisha na katika maonyesho makubwa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...