Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na viongozi wa mkoa Kilimanjaro baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kilimanjaro Julai 20, 2014 kwa ziara ya siku moja wilayani Same.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka jiwe la Msingi la Chuo cha Ufundi ( VTC) cha Maore wilayani Same Julai 21, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Jaji Mstaafu, Amir Manento baada ya kukabidhiwa nyumba iliyojengwa na Jaji huyo kama mchango wake kwa Wananchi wa kijiji alichozaliwa cha Mtii. Nyumba hiyo ilitolewa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Same ili ilitumike kama makazi ya Walimu. Julai 20, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na watoto wa kijiji cha Mtii wilayani Same baada ya kukabidhiwa nyumba ya walimu iliyojengwa katika kijiji hicho na Jaji Mstaafu Amir Manento, Julai 20, 2014.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akipanda mti katika eneo la kijiji cha Mtii wilayani Same
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (kushoto) akipokea zawadi ya miwa kutoka kwa mkazi wa kijiji cha Mtii wilayani Same (jina Halikupatikana) baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda akupokea nyumba iliyojengwa na Jaji Mstaafu, Amir Manento ikiwa ni makazi ya walimu kijijini hapo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...