Katika kuendeleza wajibu wake wa kutoa mafunzo ya muda mfupi, Chuo cha Diplomasia kimeendesha mafunzo ya juma moja ya Itifaki na Uhusiano ‘PROTOCOL AND PUBLIC RELATIONS’ kati ya tarehe 18 – 22 August, 2014. Mafunzo haya yalilenga kuwaongezea uwezo maafisa mbali mbali kutoka serekalini na sekta binafsi. Mafunzo haya ni muendelezo wa mafunzo  ya muda mfupi yatolewayo na Chuo cha Diplomasia kila mwezi, 

katika mafunzo hayo ambayo Kwa kawaida wawezeshaji wa mafunzo hayo ya muda mfupi katika Chuo cha Diplomasia, huwa ni mabalozi na wakufunzi waliobobea katika mambo ya Diplomasia na hivyo kuwapa washiriki uzoefu na mafunzo ya kiutendaji zaidi ili kuwajengea uwezo na ufanisi katika kuboresha majukumu yao. 
 PICHA YA WASHIRIKI WAKIWA NA BALOZI SANGA ‘mwenye Kaunda suti katikati’

Mafunzo hayo yalihusisha maofisa wa kada mbalimbali kutoka idara za Serikali, Chuo cha Ardhi, Jeshi la Wananchi, Magereza, Ubalozi wa Uingereza, na sekta binafsi kama Benki Kuu ya Tanzania, SMART TANZANIA (Telecom), SERENA HOTEL, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Chuo cha Utalii Tanzania,  Idara ya Uhamiaji, Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Umoja wa Mataifa (UN),

Mafunzo hayo ya juma moja yaliyofanyika Kurasini Dar es salaam, washiriki walijifunza jinsi ya kuratibu itifaki za dhifa, sherehe za kitaifa na mikutano mingine mbali mbali. Pia walijifunza Diplomasia, uhuisiano wa umma na namna bora ya kuandaa taarifa kwa ajili ya mawasiliano na umma.
Picha ya Pamoja.

Akifunga mafunzo hayo, Mkuu wa Idara ya Utafiti, Uchapishaji, Ushauri na Kozi fupi, Bw. Juma M. Kanuwa alisisitiza kwamba mafunzo hayo yatawasaidia maofisa hao kuboresha utendaji wa kazi zao.

“Kazi zinazohusiana na itifaki na uhusiano wa umma (Protocol and Public Relations) zinahitaji utaalam ambao utamfanya mtu aweze kutimiza majukumu yake kwa ufasaha na kufikia malengo na matokeo mazuri. Hivyo mafunzo haya ya Itifaki na mengine yote yanayotolewa na Chuo cha Diplomasia yana lengo la kuwajengea uwezo na utaalam washiriki wote ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi na kupata matokeo bora,” alisema.
Akaongeza kuwa, kutokana na uhitaji mafunzo haya  yatarudiwa tena Zanzibar mnamo mwezi wa kumi, yakifuatiwa na ‘INTERNATIONAL SECURITY AND ARMS CONTROL,  FRENCH LANGUAGE na DATA COLLECTION AND ANALYSIS (Using SPSS,SQL and STATA) hapa chuo cha Diplomasia, na kuwataka wale wote wanaohitaji wafike chuoni ama kupiga namba 0713667303 au cfrshortcourse@yahoo.com kwa maelezo zaidi na kupewa utaratibu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...