Mpendwa
Baba yetu, Joseph Mturi Mahemba
Hatimaye siku, Miezi imepita
hadi hii leo ambapo imetimia Miaka miwili (2) tangu ulipotutoka ghafla usiku
ule wa siku ya jumatano ya tarehe moja ya Mwezi Agosti, 2012 na kutuachia
huzuni kubwa.
Japokuwa haupo nasi hapa duniani lakini tupo
nawe kiroho kwa kuendeleza mema yote uliyotufundisha na kutuasa.
Tunakukumbuka kwa Upole,
Upendo, Busara na Ukarimu uliokuwa nao kwa familia na Marafiki. Mwongozo na
matendo yako yataendelea kuwa dira kwetu.
Daima unakumbukwa sana na
Mkeo Rose Joseph, dada zako Theresia,
Karaghita, Wankuru na Mnaga, wanao wapendwa Michael, Mkami, Niwa, Sagana, Mary,
Geofrey, Nyakaho, Lecardia na Pricilla, na wajukuu zako wote.
Ibada Maalum ya Maombi itafanyika
tarehe 03/08/2014 Saa 2.00 asubuhi kwenye kanisa katoliki la Mt Maurus
Kurasini, Dar es Salaam.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa
jina lake libalikiwe.
Poleni ila mwaka 1955 hapo juu ni sahihi?
ReplyDelete