Na Maregesi Paul
SIKU
moja nilikuwa katika mkutano wa Jukwaa la Wahariri ambao mgeni rasmi
alikuwa Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginard Mengi.Katika mazungumzo
yake, Mengi aligusia historia ya maisha yake ambapo alisema alikulia
katika familia masikini.Kwa mujibu wa Mengi, nyumba aliyokulia ilikuwa
na panya wengi pamoja na mende na kwamba kila walipokuwa wakilala usiku,
wapita njia walikuwa wakiwaona kwa sababu nyumba ilikuwa imejaa matobo.
Pamoja
na mazingira hayo, Mengi kwa sasa ni kati ya matajiri wakubwa
wanaoheshimika ndani na nje ya nchi na suala la umasikini aliokulia,
limebaki kuwa historia.Hivyo hivyo, hata mimi niliyeandika makala haya,
niliwahi kuvua dagaa na sangara kwa kutumia nyavu haramu ziitwazo
makokoro. Lakini sasa mimi ni mhariri wa gazeti hili na suala la uvuvi,
limebaki katika historia.
Wakati
hayo yakitokea, katika Radio Clouds kuna watangazaji wengi wanaovuta
masikio na hisia za wasikilizaji kutokana na lugha na vichekesho
wanavyovitumia pindi wanapokuwa studio.
Miongoni mwao ni Said Seleman maarufu kwa jina la Mbwiga wa Mbwiguke.
Kama
ilivyo kawaida kwa watu kuwa na historia tofauti tofauti kama
nilivyoeleza hapo awali, wakati wa mahojiano maalum na MTANZANIA
Jumatatu, Mbwiga anaeleza kwa kirefu ni wapi alikotokea hadi akawa mmoja
wa watangazaji maarufu katika radio hiyo maarufu nchini.
“Kwanza
nianze na maana ya jina Mbwiga. Mbwiga ni neno la kizaramo ambalo maana
yake ni rafiki. Kwa hiyo mimi ni rafiki wa kila mmoja kwa sababu huwa
napenda sana kuwachekesha watu.
“Lakini pia, maisha ni mzunguko na kamwe hakuna binadamu anayezaliwa na kujua maisha yake yatakuwaje kwa siku zijazo.
“Kwa
maana hiyo, hiki nitakachokieleza ndivyo kilivyo kwa sababu hapa nilipo
sikutarajia kama itatokea siku nikawa mmoja wa watu wanaoungwa mkono na
mamilioni ya Watanzania.“Kwanza kabisa niseme tu kwamba, mtu
aliyenifikisha hapa ni mtangazaji mwenzangu aitwaye Shafii Dauda. Huyu
ndiye aliyenileta Clouds baada ya kuniona naweza kuwa na mchango fulani
fulani katika redio yetu hii.
“Sikumbuki
ni mwaka gani, lakini nakumbuka ni kama miaka mitatu iliyopita, siku
moja usiku nilikuwa pale Muhimbili Shule ya Msingi kwenye mazoezi ya
mpira unaowahusisha wachezaji wakongwe kama akina Akida Makunda, Mohamed
Binda, Idd Moshi, Ally Mayai, Crement Kahabuka, Dua Said na wengineo
wengi .
“Siku
hiyo nilikuwa sichezi bali nilikuwa shabiki tu nikiwashangilia wenzagu,
kwa hiyo, mazoezi yalipomalizika, Shafii Dauda alikuja mahali
nilipokuwa na akina Ally Mayai na alitukuta tunacheka,” anasema Mbwiga
na kuongeza.“Alipoona tunacheka, akauliza tunacheka nini, Ally Mayai
akamwambia huyu jamaa anatuchekesha, hebu mchukue umtumie kwenye kipindi
chako kile cha michezo cha saa tatu usiku atakusaidia sana,” anasema
Mbwiga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...