Mhe. Omar Mjenga, amekutana na Mhe. Hamad Buamim, Rais na Mtendaji Mkuu wa Dubai Chamber of Commerce and Industry na kufanya naye mazungumzo.

Katika mazungumzo, wamejadiliana uwezekano wa kuwa na ziara ya kibiashara kwenda Tanzania, kwa makampuni na viwanda vilivyopo Dubai, ili kukutana na wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda Tanzania, ili kujionea na kuibua fursa za uwekezaji. Wamekubaliana ziara hiyo ifanyike mwanzoni mwa mwaka kesho na hivyo basi kuanza maandalizi mapema.

Mwezi Novemba, kutakuwa na ziara ya kibiashara ya makampuni kutoka Falme ya Ajman.

Aidha, wamezungumzia kuhusu mkutano wa Africa Global Business Forum utakaofanyika tarehe 1-2 Oktoba 2014 hapa Dubai. Mtukufu Sheikh Mohammed bin Rashid al Maktoum amemwalika Rais Kikwete kuhudhuria pamoja na marais wengine wa Mali, Ghana, Uganda, Mozambique, Ethiopia, Senegal, Burkina Faso, Sudan na Ivory Coast.

Mkutano huu hufanyika kila mwaka ambao huzungumzia njia muafaka ya ushirikiano kati ya Serikali ya Dubai na UAE kwa ujumla na nchi za Afrika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. does this guy work or is a meetings man

    ReplyDelete
  2. Huyu jamaa kila siku tunaona humu kakutana na huyu mara huyu tungependa kuona tija ya hiyo mikutano yake

    ReplyDelete
  3. Huyu ni mtu mwenye kipaji!
    Anaweka mazingira yatakavyo ki biashara na investment. Ila naona hamna faida huko maana hawa IMPLIMENT!
    Huyu kijana afaa kuwa waziri!
    Al Mahruqi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...