Mfalme wa nyimbo za asili nchini Tanzania Costa Siboka, Baada ya kufanya kufuru na kuvunja Rekodi katika Miji ya Mwanza, Geita,Visiwa vya Ghana na Ukerewe Sasa anatarajia kumalizia ziara yake katika Miji ya Bunda,Bariadi,Shirati,Tarime , Butiama na Dutwa.Shoo hizo zitafanyika tarehe 22 Septemba 2014 mpaka tarehe 30 septemba 2014.Mfalme Siboka akiwa na kundi lake ametamba na kusema yeye in jeshi la Mtu mmoja...Hakunaga shiiida, Vuta raha Barimi tumpokee Mfalme.Siboka yupo katika utambulisho WA nyimbo yake mpya Engele yange aliouimba kwa lugha za makabila manne.Kisukuma,Kihaya,Kikerewe,Kijita na Kikurya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Inapendeza sana na ni fakhari kubwa sana kuzienzi na kuziendeleza nyimbo zetu za asili. Mbali ya kuwa ni mojawapo ya burudani kama zilivyo nyingine, lakini pia inatambulisha tamaduni, mila na desturi za jamii au kabila husika, kitu ambacho ni kizuri kujivunia. Hongera sana Costa Siboka, Umenifanya nimkumbuke marehemu Mr. Ebo (R.I.P.) na ule wimbo wake..Mi Mmasai...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...