MSANII wa Muziki wa Kizazi kipya nchini,Naseeb Abdul  maarufu kama Diamond Platnumz amehojiwa na Jeshi la Polisi baada ya kuonekana na mavazi halisi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika Tamasha la Fiesta lililofanyika jijini Dar mwishoni mwa wiki.

Diamond amejikuta hapo  siku moja tu baada ya Meneja wake Babu Tale kukamatwa  jana kwa kuhojiwa na kulala mahabusu kuhusiana na matumizi hayo ya mavazi ya kijeshi katika onyesho la Fiesta.
Habari zinasema Diamond naye alijisalimisha mwenyewe polisi ambako baada ya mahojiano aliachiwa kwa dhamana. Magwanda aliyokuwa nayo aliyakabidi polisi wakati uchunguzi ukiendelea.

Habari zaidi zitafuata.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. Haya mavazi yanauzwa masokoni. Sasa shida ipo wapi?

    ReplyDelete
  2. Hata sumu inauzwa dukani shida ni kuinywa!

    ReplyDelete
  3. Hawana kazi ya kufanya hao

    ReplyDelete
  4. Solo lipid libalouza share za jeshi? Acha kutuongopea bwana; do go kachemka huyo

    ReplyDelete
  5. JWT lilishakataza watu wa uraiani kuyavaa!

    Tiini, hakutakuwa na taabu!

    ReplyDelete
  6. Jamani sasa naona wamekosa kazi. Jamani uniform ni mavazi tu. Sioni tatizo la mtu kuvaa apendacho. Nendeni mkawakamte vibaka na wanaovunja sheria za muhimu sio watu watu wasio na hatia. Inatia aibu sasa kwa d kweli. Mtg kama huyu kijana mdogo Diamond anajaribu kujitafutia maisha ya haki, hajaiba kwa mtu, badala ya kumpa muongozo mnamzalilisha kwa ajili tu ya mavazi ya mfano wa jeshi. Wapi tuendapo watanzania?

    ReplyDelete
  7. Mdau wa hata sumu inauzwa dukani shida ni kuinywa. Umenichekesha sana.

    ReplyDelete
  8. That is not fair, wearing jeshi cloth it is doesn't mean he is a criminal. Leave him alone.

    ReplyDelete
  9. Majeshi ya wenzetu yanarusha rockets au kutuma satelite angani sie karagabaho...ivi hawana taarifa kwamba nguo hizo zapatikana mtumbani??? au kila chenye madoa doa ni zao?? Ukraine wafanyakazi wa sewage wanavaa magwanda ya jeshi au wakata nyasi kawaida mbona jama.....ebu tufikirie mambo makubwa jamani tuache....

    ReplyDelete
  10. Tatizo la DIAMOND ni tatizo linalowasumbua wasanii wengi wa kibongo, MENEJIMENTI MBOVU. Na kwa kuwa watu kama yeye wanapoona wanafanikiwa wanaamini mbinu zao ni sahihi. Basi tungojee, maana NGOMA IKILIA SANA, HAICHELEI KUPASUKA

    ReplyDelete
  11. Police in Bongo have nothing to do apart from kupokea rushwa. Hapa nilipo hayo mavazi yanapatikana kila mahali, kuna yale ya bei ya juu and u get them in Departmental Stores au yale cheap ambayo unanunua sokoni. Polisi na nyie jeshi endeni na time, hatuko karne ya 19 sasa. Huyo ni msanii he can wear what fits the occasion. Wake up Bongo.

    ReplyDelete
  12. Mbona nchi nyingine zote duniani raia wake wanavaa nguo hizi?? wanataka kusema kuzivaa ndio kuteka nchi? hii inaonesha waziwazi kukosa watu wanao fikiria na kukosa busara, tunahitaji mfikirie kuhusu kurusha rocket au kutengeneza silaha zenye masafa ya mbali na sio mdebwedo wa kununua tu! Uhuru wa raia na demokrasia naona unaingiliwa na jeshi yote haya kwasababu hawana kazi ya kufanya au tuambieni kabisa kama hii nchi inaendeshwa kijeshi tujue kabisa.

    Tuachieni uhuru wetu. Na Mbaki kufikiria kuilinda nchi tu. Mwacheni Diamond huru, Wahisani msaidieni Diamond na raia watz.

    ReplyDelete
  13. Mbunge wetu na waziri wetu mtarajiwa Mh Ankali Michuzi tunakuomba msaidie Diamond na kuitetea hoja ya kuzivaa hizi nguo.

    ReplyDelete
  14. JWTZ walishatoa waraka kuwa mtu binafsi haruhusiwi kuvaa mavazi ya jeshi kwani yanatumika sana kwenye uhalifu, mbona wengi tu wanaadhibiwa kwa kosa hilo, kwani yeye diamond ndio awe juu ya sheria, noo! kosa ni kosa ngoja aadhibiwe, next time atajifunza.

    ReplyDelete
  15. no one is above the law, aadhibiwe tu, then atajifunza kufuata sheria.

    ReplyDelete
  16. KWA KWELI TANZANIA BADO TUPO NYUMA SANA, HIZO NGUO NDIO ZA KUMFANYA MTU NI KRIMINAL TAYARI?

    HIYO NI FASION KATIKA FANI YA MUSIK YA VIJANA WA KISASA NA NI DUNIA NZIMA WANAVAA NGUO HIZO SIO LAZIMA UWE UNAFANYA KAZI ZA JESHI TU . MIMI MWENYEWE NINA FULL COMBAT PAIR 3 NA NINA ZIVAA MPAKA MSIKITINI MBONA HASHANGAI MTU. DIAMOND ALIKUWA ANACHANGAMSHA SHOW YAKE KWA SABABU HIO ILIKUWA NI EVENT KUBWA KATIKA MAISHA YAKE,HATUWEZI KUCHAGULIA AVAE NINI NA NINI ASIVAE. TANZANIA WAKE UP SASA TUKO MIAKA 12 BAADA YA MELLENIUM. MAMBO YA NYERERE YAMEISHA PITA

    MDAU COPENHAGEN

    ReplyDelete
  17. ni huko Copenhagen na TZ ina sheria yake. Kila nchi inaendeshwa kwa sheria ya nchi husika, la muhimu ni kutii sheria.

    ReplyDelete
  18. Hapa Tanzania sio nchi za nje!! Sheria na amri ya jeshi ni kwamba raia haruhusiwi kuvaa nguo za jeshi au zinazofanana na magwanda ya kijeshi!

    Hata hao wauzamitumba ukiwauliza watakwambia hairuhusiwi kuagiza na kuuza nguo zinazofanana na za kijeshi (kama vile hawaruhusiwi kuagiza nguo za ndani kama chupi, sidiria, n.k.)

    Angeomba kibali kama walivyofanya East coast Army akina Krazy GK, AY, Mwana FA katika ile video ya Komaa Nao kama sikosei - waliomba ruhusa na walikubaliwa.

    ReplyDelete
  19. Ipo clear kwamba serikali imesha tangaza kuwa mavazi ya jeshi na polisi ni marufuku kuvaliwa na raia, hata kama nchi nyingine watu wana vaa ila huwezi uka copy na ku pest maana kila nchi ina shiria na taratibu zake za utawala. Tii sheria bila shuruti, au mtapata matata buree kwa ubishi, by the way huwezi sare ya jeshi ukakatikie viuno stajini, ni dharau.

    ReplyDelete
  20. I can understand kwa nini maafande hawapendi watu wavae hayo magwanda. Kwa ufupi wanataka kutuondelea watu wanaovaa hizo nguo na baadaye kutudhulumu. Basi ni kusema kuwa wanafikiri sisi kidogo wapumbavu na tunahitaji msaada tusipokorowe na wajanja. Basi lini tutaamka?

    ReplyDelete
  21. ...Huwezi kuilinganisha Tanzania na nchi zilizoendelea kama USA na nk. katika nchi ambayo bado watu wanaamini kuwa watu wanatembea na Noah (aina ya Gari) nyeusi wananyonya damu za watoto, na kumwita kila mtumishi wa Hospitali Daktari (regardless ni nesi, muhudumu, lab technologist etc) huwezi kuruhusu nguo za jeshi kuvaliwa mitaani.

    ReplyDelete
  22. Hayo maduka yanayouza hizo nguo pia yakamatwe

    ReplyDelete
  23. Mkuu uliyesema kwamba East Coast walipewa kibali cha kuvaa magwanda, si kweli. Walikuwa wabishi tu, mpaka leo King GK bado anavaa nguo kama za jeshi. Wanajeshi waliwaheshimu tu kwa vile waliwapenda. Kwenye Ama zao ama zangu, producer alikuwa mzungu toka South Afrika, aliwalia ngumu wanajeshi walipoenda kumnyanganya hizo nguo za jeshi GK, na jeshi likafyata(ndiyo stori ya ndani). Kusema kweli sioni tatizo kwa mtu kuvaa hizo sare, kuwe na sare au si sare, uhalifu utakuwepo, na majambazi watavaa sare wakitaka. Siye wabongo tumefika kikomo wa ubongo wetu kutatua matatizo makubwa, tunatafuta michepuko ili watu wasahau vitu muhimu. Basi hata wanaogiza kuiba benki wakamatwe, maana hata Wasanii wanaoigiza si wamevaa sare za JWTZ?!! Pole TZ.

    ReplyDelete
  24. Kama sheria ya nchi hairuhusu hayo mavazi uraiani basi kijana aadhibiwe. Vitu kama hivi mkianza kulegeza sheria zote zitavunjwa na itagharimu serikali. Vitu kama hivi mdio vinaanza kidogo kidogo mwishoni nchi inakosa mwelekeo. Tafadhali watanzania jivunieni nchi yenu msiige vituvya mataifa mengine. Kamamtu anataka kufanikisha zaidi tukio lake kwa ktumia vitu ambavyo viko nje ya sheria aombe kibali. Watanzania tuwe macho na mabadliko ya ulimwengu huu. Mvhangiaji aliyetoa mfano kwa kutumia sumu ndugu yangu jitahidi kutumia mifano yenye matumaini.

    ReplyDelete
  25. Kama shrie ipo na mtu amevunja anatetewa nini. Kijana aelimishwe pengine alijisahau na hapo hapo adhabu yake kwa vyovyote inajulikana wakati hiyo sheria inatungwa basi itolewa ili iwe mfano tujue kweli mtu akivunja sheria anapaswa aadhibiwe na sio wasuesue mwishoni usikie kimya. Tena tunasubiri kwa hamu tujue hatima yake.

    ReplyDelete
  26. rashid richieOctober 24, 2014

    nchi nyengine watu wanavaa kama nguo za kawaida ila tofauti ni vyeti vya kazi hiyo,,mshangao nchi zetu za Afrika

    ReplyDelete
  27. Ignorance is not an excuse to the law

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...