Wingi wa pikipiki na baiskeli katika mji Mkuu wa Vietnam, Hanoi, ni balaa. Yeyote aliyewahi kutembelea mji huo mkongwe anakiri kwamba songombingo la pikipiki na baiskeli si la kawaida, hasa ikiwa unatembea kwa miguu. 
Takwimu rasmi zinasema kulikuwa na pikipiki milioni 4 mwaka 1996 katika Vietnam yote. Leo idadi hiyo ipo mjini Hanoi peke yake, ambapo inaaminika kuna jumla ya pikipiki milioni 39 nchi nzima, ikimaanisha kwamba, ukiondoa wazee sana, na watoto, karibu kila M-Vietnam ana yake. 
Leo Ankal,  aliyeko Hanoi, mji ambao umekuwa na wakaazi tokea miaka 3000 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu, kashuhudia hali hiyo katika mtaa mmoja sehemu za Hanoi ya zamani. Mambo ndio kama hivi…

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Uzuri wake hazitumiki ujambazi,zinatumika kupunguza msongo wa magari

    ReplyDelete
  2. ...afu hakuna ajali wala kugongana..ni ustaarabu tuu.. wote wana haraka na kuheshimiana.

    ReplyDelete
  3. N NIDHAMU YA HALI YA JUU HAKUNA MBWEMBWE WALA USHAMBA WA KUPIGA VIBUYU NA MASPIDI YA AJABU YA WATANZANIA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...