Kivuko cha Msangamkuu( MV Mafanikio) chenye uwezo wa kubeba uzito wa tani 50 pamoja na abiria 100 kikiwasili Mkoani Mtwara tayari kwa kuanza kazi rasmi ya kutoa huduma kati ya upande wa Mtwara Mjini na Msangamkuu.
Kivuko kipya cha (MV Mafanikio) kama kinavyoonekana mara baada ya Serikali kutekeleza ahadi yake ya kuwaletea wananchi wa Mtwara Kivuko hicho kipya.
Wananchi wakikimbia kuingia ndani ya Kivuko hicho kipya cha (MV Mafanikio) huku wakishangilia kuonyesha furaha yao mara baada ya kivuko hicho kuwasili mkoani Mtwara.
Baadhi ya kina mama nao walipata fursa ya kukaa na kufurahia ndani ya kivuko hicho kipya.
Usafiri huu wa Mitumbwi ndio uliokuwa unategemewa na wananchi hao wa Mtwara kabla ya ujio wa Kivuko kipya cha Msangamkuu.
Mkurugenzi wa Ufundi na Umeme (DTES) Dkt. Wiliam Nshama kutoka Wizara ya Ujenzi akipita kukagua Kivuko hicho kipya cha Mv Mafanikio. Picha zote kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Ujenzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Madhari ya Mtwara yanaonekana vizuri sana. Panaweza hata kufaa kwa Utalii ikiwa kuna hoteli zenye hadhi ya kimataifa.

    ReplyDelete
  2. kinafanya kazi toka wapi hadi wapi hicho kivuko? na hiyo msanga mkuu ndio ina maana ya mafanikio? mbona kama maana ya hilo neno iko tofauti? kimetoka wapi? hebu mtujuze

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...