Mtangazaji wa zamani wa Radio Tanzania (RTD) sasa TBC,Ben Hamis Kikoromo maarufu kama Ben Kiko enzi za uhai wake akiwa katika moja ya semina alizohudhuria.

MTANGAZAJI na mwandishi wa habari mkongwe nchini Ben Kiko amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hosptali ya taifa ya rufaa ya Muhimbili jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Ben Kiko ambaye jina lake kamili ni Ben Hamisi Kikoromo alihamishiwa katika hosptali ya Muhimbili kutokea hosptali ya Jeshi ya Milambo ya mkoani Tabora ambako alilazwa kwa ajili ya matibabu ya figo kwa muda wa wiki mbili.

MUNGU ILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA,
AMIN
Mtangazaji wa zamani wa Radio Tanzania (RTD) sasa TBC, Ben Hamis Kikoromo maarufu kama Ben Kikoakizungumza na Mwakilishi wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini Dixon Busagaga alipomtembelea nyumbani kwake eneo la Cheyo mkoani Tabora wakati wa uhai wake.


Mtangazaji wa zamani wa Radio Tanzania Dar es salaam ambayo sasa ni TBC Taifa, Ben Hamis Kikoromo (pichani akiwa ameshika hati ya Tuzo ya Utumishi uliotukuka wa Maisha April 2012) maarufu kama Ben Kiko,   

 atakumbukwa kama mmoja wa watangazaji mahiri ambao walijipatia umaarufu mkubwa ambapo katika enzi za uhai wake alifanya makubwa wakati wa Vita vya Kagera kwa kuleta matukio mbalimbali kutoka uwanja wa vita. Pia aliupaisha sana mkoa wa Tabora alikokuwa akifanyia kazi kwa habari na visa mbalimbali katika kipindi cha RTD cha Majira.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. R.i.p Ben Kiko

    ReplyDelete
  2. R.I.P Ben Kiko hakika sitakusahau kwa jinsi ulivyo tuhabarisha ita vya Kagera 1978-1979 kwa weledi wa hali ya juu

    ReplyDelete
  3. mungu ailaze roho yako peponi

    ReplyDelete
  4. R.I.P Ben Kiko.
    Tutakukumbuka kwa utangazaji wako mahiri na machachari hasa kwenye kipindi cha majira.

    ReplyDelete
  5. Eh kwa sisi wa zamani enzi za RTD tulikuwa tunapenda sana kukusikiliza jinsi ulivyokuwa unahabarisha na kutufurahisha kwa wakati mmoja.

    Maana utangazaji wa marehemu Ben Kiko ulikuwa wa aina yake peke yake, ukiwa umenuna utacheka tu.

    RIP Ben umetangulia na sisi tuko nyuma.

    ReplyDelete
  6. Duh jembe limepotea jina la bwana lihimidiwe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...