Bw. Clement Ngosha wa kijijini Kabita Wilayani Busega, Simiyu, akitumia mbegu za
mahindi kueleza hali ya chakula kijijini hapo kwa wataalam wa Tathmini ya Hali ya
Chakula na Lishe inayofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Oktoba, 2014.
Mtaalam wa Usalama wa chakula kutoka Wizara ya kilimo, chakula na Ushirika, Bi. Tatu
Kayumbu akiihoji moja ya kaya kijijini Mwamanyili,Wilayani Busega, Simiyu wakati wa
Tathmini ya Hali ya Chakula na Lishe inayofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu kijijini hapo,
Oktoba, 2014.
Baadhi ya wanakijiji wa kijiji cha Kabita wilayani Busega, Simiyu wakifuatilia mkutano
wa kijiji uliokuwa ukijadili hali ya Chakula na Lishe kijijini hapo wakati Ofisi ya Waziri
Mkuu ilipofika kijijini hapo kufanya tathmini ya masuala hayo Oktoba, 2014.
Na. Ibrahim Hamidu
Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya Uratibu wa maafa inafanya Tathmini ya Hali ya Chakula na
Lishe Mkoani Simiyu katika Wilaya zake zote ambazo ni; Halmashauri za Wilaya za Bariadi,
Itilima, Maswa ,Bariadi Meatu na Busega.
Akiongea mkoani Simiyu kiongozi wa Wataalam wa tathmini ambaye pia ni mratibu wa shughuli
za maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Edgar Senga alibainisha kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu imefikia
maamuzi hayo ya kufanya tathmini mkoani Simiyu baada ya mkoa huo kutuma maombi katika
Ofisi hiyo kuwa wana upungufu wa chakula.
“ Ofisi ya mkoa ya Simiyu ilileta maombi kwa ofisi ya Waziri Mkuu kuwa wanaoupungufu wa
chakula takribani tani 48,975, kwa kuwa Ofisi yetu ndio yenye dhamana ya kuratibu misaada
ya chakula hivyo haikuwanabudi kufanya tathmini ya haraka ili kubaini hali ya chakula ya mkoa
huu ili kuweza kuamua namna ya kushughulikia maombi yao ya msaada wa chakula” alisema
Senga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...