Ifuatayo ni update ya msiba wa mdogo wake Mwenyekiti wa African Stars Entertainment (ASET) Baraka Msiilwa, Marehemu Furaha Ramadhani Baraka, kilichotokea wikiendi iliyopita huko Ubelgiji.


Taarifa ni kwamba mwili wa Marehemu mdogo wetu Furaha unaondoka Brussels kesho  usiku kwenda Zurich. Utalala Zuruch na kusafirishwa Jumatano Asubuhi kwa ndege ya shirika la Swiss Air, na unatarajiwa kuwasili Dar es salaam siku  hiyo hiyo ya Jumatano mnamo saa mbili usiku

Mazishi yamepangwa kufanyika siku ya Alhamisi  milango ya Alasir katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam baada ya kuuswaliwa katika Mskiti wa Maamur Upanga. Msiba upo nyumbani kwa marehemu mama yetu Kinondoni Hananasif/ Mkwajuni hapa Dar es salaam. 

Habari hizi ziwafikie ndugu, jamaa, jirani na marafiki popote pale walipo. Tuzidi kumuomba Mola aiweke roho ya mareheme mahala pema peponi

 - AMIN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...