Balozi  Tuvako Manoni ( nyuma) akiwa katika picha pamoja na  wanafunzi wenye umri kati ya miaka 11-14 kutoka shule  za Montessori waliofika katika Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni sehemu ya ziara ya  Mafunzo yao  yanayolenga kuwajengea uwezo wa kujielimisha kuhusu masuala mbalimbali yanayoendelea katika Umoja wa Mataifa. Katika ziara hiyo pamoja na kutembelea Makao Makuu ya  Umoja wa Mataifa pia hutembelea  baadhi ya Wakilishi za kudumu  kwa lengo la kutaka  kufahamu vipaumbele vya nchi hizo na ushiriki wao katika   mijadala mbalimbali ya Umoja wa Mataifa na pia hupenda kujifunza  historia ya nchi hiyo.  katika picha wapo pia walimu walioambatana nao katika ziara hiyo. Anaoneka pia Afisa wa Uwakilishi wa Kudumu . Bw. Noel Kaganda  anayeratibu shughuli za Baraza  Kuu la Umoja wa Mataifa  na ambaye alipewa jukumu la  kuwaeleza wanafunzi hao na walimu wao vipaumbele vya Tanzania katika Umoja wa Mataifa pamoja na kujibu  maswali mbalimbali kutoka kwa wanafunzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...