Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali Mhe Zitto Kabwe akisoma Ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (GAG) kuhusu akauti ya ESCROW Bungeni Mjini Dodoma leo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Anne Makinda akifafanua jambo wakati akiendesha Bunge hilo leo mjini Dodoma.
Baadhi ya wahudumu wa Bunge wakigawa Ripoti ya GAG kuhusu akauti ya ESCROW kwa Wabunge
Waheshimiwa Wabunge wakipitia ripoti ya GAG kwa makini wakati ikisomwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Mhe Zitto Kabwe.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Imekuaje leo tunasoma hii habari hapa!!!

    ReplyDelete
  2. Jamani, hivi ufisadi wa Bongo una dawa yake. Wakifishitakiwa na kufisiliwa labda itakuwa fundisho kwa sisi wote.

    ReplyDelete
  3. hata majaji, oohhh mimi sina la kusema zaidi!

    ReplyDelete
  4. Ni kugawana tu mabilioni yetu, nangojea kusikia watakavyojitetea. Nchi zingine hao wangekuwa tayari Keko au Ukonga. Yaani kweli Muhimbili hakuna dawa lakini wao wanagawana mabilioni ambayo yangeendesha Muhimbili kwa miaka mitano.

    ReplyDelete
  5. Kweli mwacheni Mungu aitwe Mungu, leo Mungu anataka kuwaonesha wanyonge wanaozulumiwa na watu haki zao. Haki kweli kumbe Tanzania tunaweza kuwa matajiri kuyazidi hata mataifa matajiri hapa duniani endapo tu kusingekuwa na huu ufisadi. Hivi najiuliza ni kwa nini watu wanapenda pesa kiasi hicho? mbona hizo pesa ni nyingi sana kwa mtu mmoja jamani. Fikiria watu wanakufa mahospitalini, kweli mtu anaenda kupokea peza kwenye gunia? huu sio utani kwa Muumba kweli. Maaskofu wanajua kabisa kuwa ulafi ni mzizi mkuu wa dhambi, leo hii utamuhubiria nani aache kula rushwa, aache uizi, aache ulafi kama wewe ni namba moja? tumwogope Mungu. Naomba msinibanie maoni yangu wahusika

    ReplyDelete
  6. Si kawaida yangu kutoa ujumbe kwa njia hii. Lakini kwa umuhimu wake, Napenda kumshukuru mdau aliyeshangaa kukuta habari hii hapa.
    Kwa ujumla sera za Globu ya Jamii hazifungamani na upande wowote wa kisiasa, kidini ama ki-hisia, na daima tutarusha habari zilizo rasmi na zilizotoka katika vyombo ama taasisi rasmi. Tunashukuru kwa kuwa nasi na kupata habari yenye uhakika. Ubarikiwe sana

    ReplyDelete
  7. Taarifa hii inatisha. Mungu atuepushe tusijekuwa a Mafia State. Mafia State inahusu uhalifu unaojumuisha Viongozi wa Dini wa Kisiasa, Wanasheria, Wafanyabiashara na Wahalifu. Escrow akaunti imejumuisha wote hawa. Tunaomba Mungu atujalie na kumpa Mhe. Rais busara ya kutunuru na kurejesha imani kwa Uongozi na utawala wa Nchi yetu.

    ReplyDelete
  8. Baada ya EPA Bunge lilitunga sheria yoyote kudhibiti utoaji wa pesa nyingi Benki kuu bila idhini yake? Kama halikufanya hivyo huu ni wakati muafaka ili isiwe tu bunge linaingia baada ya matujkio kufanyika.

    ReplyDelete
  9. MHM!!! kila mtu mwizi, hata sisi ni wezi, yawezekana tusiibe hela, lakini ni wezi kwa namna Fulani, hivyo basi, asiyekuwa mwizi kwa namna yoyote ile, na awe wa kwanza kumhukumu mwenzie.

    ReplyDelete
  10. Yaani wanadamu ni watu wa ajabu sana, tunajidai oho, wamekula mabilioni yetu, lakini ukitaka kujijua wewe ni safi, upewe hapo gunia la pesa ulilinde, kwa muda wa miaka kadhaa, je utavumilia kuliangalia muda wote bila kunyofoa senti?, watu waaminifu ni wachache sana duniani, ni wa kuhesabika. hawa wamegundulika kwa sababu wizi wao ni wa mahela makubwa, fikiria wewe au mimi ninayeiiba kidogo kidogo, Je? piga hesabu ni mabilioni mangapi umeiibia serikali? kama kuna dhambi ambayo ni mbaya sana ni kuhukumu watu, tunatakiwa kujihukumu wenyewe, je ni wasafi? kama sio msafi, usijaribu kuhukumu mtu. ukihukumu utahukumiwa.

    ReplyDelete
  11. Hoja zinapanguliwa ile mbaya.... Madeni yamegeuka kuwa hela lini? Hii taarifa imeharakishwa mnooo

    ReplyDelete
  12. Inauma sana kuona kuwa viongozi wetu ndio wanaotuibia tena huku wanajua. Mungu atawahukumu ila kwanza wafilisiwe ili wengine wajifunze.

    ReplyDelete
  13. Prof. Muongo/Muhongo Sospeter ameeleza vizuri lakini aliyoyasema kwa mujibu wa taratibu ndiyo yaliyofanyiwa uhakiki na yakaonekana kuwa ni madudu, sasa sijui Watanzania wezangu tukae wapi kimtazamo maana kila mmoja muongo na mhuni kuliko mwengine. ninavyoamini na simlazimishi mtu yeyote kuamini kama ninavyoamini mimi kuwa Ripoti ya Serikali kupitia kwa Waziri wa Nishati ndio kiini cha Ripoti au taarifa ya Mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali, TAKUKURU na halimae Taarifa ya PAC bila ya hivyo kusingelifanyika chochote, ufahamu wangu mdogo kwa mambo haya lkn nikiwa kama Mtanzania hata kama Taarifa zote ziwe na mapungufu ONDOKENI wacheni wengine wafanya kazi kwa uwazi na uwajibikaji.Tanzania si mali yenu na mkiwa hamupo nyie wengine wapo kwanini iwe NONGWA?

    ReplyDelete
  14. Hizo pesa zirudi mala moja na hao wezi wafungwe jela

    ReplyDelete
  15. Hongera serkali kwa ufafanuzi, mwenye akili atapima.

    ReplyDelete
  16. Hata vitabu vya Mungu viliandika juu ya hatari ya fedha.
    Someni;- 1Timotheo 6:10

    ReplyDelete
  17. Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) akishatoa Tamko kuhusu Ukaguzi wa Mahesabu alioufanya , na kugundua Hitilafu au Usahihi wowote , Tamko hilo huchukuliwa kama Tamko la Serikali.Na wahusika huchukuliwa hatua za kisheria mara moja baada ya taarifa hiyo kutolewa hadharani.Ni jambo la ajabu na la kushangaza kuona , likitokea katika Bunge letu , licha ya Ripoti ya CAG kutoka na kufuatiwa na Ripoti ya PAC , bado tena Serikali inasimama katika Kizimba cha Bunge "kuikana taarifa ya serikali ileile" iliyotoka awali na kuridhiwa na serikali . Sijawahi popote Ulimwenguni hili likifanyika .Huu ni Ufisadi uliokithiri .

    ReplyDelete
  18. Niliwaambia asiyekuwa na dhambi na awe wa kwanza kumuhukumu mwenzie, umeona jana muheshimiwa "mwepesi" kumbe nae kapata mgawo bana, hahahaaaaaa. sharia ni msumeno unakata kuwili, kaazi kweli kweli. Kuna kisa kimoja kwenye biblia kinasema hivi, kuna watu walimkamata mwanamke mzinzi wakampeleka kwa Yesu ili wapate kumshitaki, walipofika Yesu akawauliza, mwamshitaki kwa kosa gani? wakasema tumemkuta anazini, Yesu akaandika chini, asiyekuwa kila dhambi ya mtu, kila anayejisoma anaondoka taratibu, mwisho akabaki Yesu na yule mama, Yesu akamuuliza washitaki wako wako wapi? unapomshitaki mtu jihakikishe wewe kwanza uko safi, maana waweza jiona mwenyewe uko safi, kumbe kuna dhambi ambayo wewe wadhani haijulikani kumbe watu wanaijua, wakakuumbua, ukabaki na aibu kubwa, na hakuna wa kukufutia labda Mungu wa mbinguni tu. kila mtu ana dhambi, sema zingine za wazi na zingine za siri. kaazzi kweli kweli

    ReplyDelete
  19. HII KALI.....hela nyingi sana hizi.
    mie nalia na Kilaini....mbona hakumshauri mwenzake yule msaidizi wa jimbo kuu la DSM namna ya kujieleza? Anasema hajui hela zilizoingizwa kwenye acc yake ni za nini anaenda kuchunguza leo! jamani....si useme unaenda kuomba ushauri kwa kilaini naman ya kujieleza?

    ReplyDelete
  20. Hakika inauma, inauma jamani, inauma sana tena sana.viongozi wakubwa ktk serikali ndio wanao tuuwa sisi wananchi wanyonge.sisi wagonjwa wa saratani, tunateseka kwa kutopata matibabu kamili hosp (Ocean Road), mara mashine mbovu, mara hakuna dawa, na km dawa ipo, je ? Unazo laki tatu za kulipia chupa moja ya 'dripu', tunasota hadi saa sita za usiku tukisubiri huduma ya mashine ya mionzi !.Mabilioni ya pesa ziko mifunikoni mwenu !(sakata la escrol). Jamani muwe na roho za kibinadam.

    ReplyDelete
  21. Na wewe nawe usilete biblia kama kigezo cha kutetea maovu. Kumbe mahakama zipo kwa sababu ya nini? haki itendeke hakuna hukumu hapa iliyotolewa ila ukweli unatakiwa upatikane. Mtawa au padre hatakiwi kuwa na account yake binafsi, anatakiwa kama amepata msaada wa pesa za jamii zipelekwe kwenye account ya jina la jimbo au shirika. Sasa pesa nyingi kama hiyo inaingiaje kwa account ya mtu binafsi wa kanisa? au na wewe ni mmoja wapo wa mgao nini

    ReplyDelete
  22. Kweli katika hali ya kawaida wakati Watanzania wenzenu wanaangaika kupata dawa mahospitalini hawapati, wanatembea kutwa nzima kutafuta maji safi ya kunywa hawapati, watoto wetu mashuleni wanakaa chini kwa kukosa madawati, au wanakaa chini ya miti kwa kukosa madarasa, watu mnagawana hela za watoa jasho bila kujali ubinadamu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...