Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

 Imeelezwa kuwa nchi ya Afrika Kusini katika bara la Afrika ndio inayoongoza kwa kuwa na njia nyingi za usafirishaji wa dawa za kulevya aina ya Cocaine na Heroine .

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,Afisa Habari wa Kituo Cha Habari wa Umoja wa Mataifa (UNIC),Stella Vuzo alisema kuwa hilo limetokana na ripoti ya Bodi ya Kupambana na Dawa za Kulevya ya Umoja wa Mataifa imeweka mkazo katika kwa nchi mwanachama kuweka mikakati katika kupambana na dawa za kulevya.

Alisema alisema nchi zilizo katika pwani za bahari zinatakiwa kuwa na uangalizi katika maeneo hayo kutokana na watu wanatumia njia hizo katika kupitisha dawa za kulevya.

Naye Mchambuzi Mkuu wa Mifumo ya Komputa wa Tume ya kudhibiti  Ukimwi DCC,January Ntisi ,amesema wanashirikiana katika kupambana na dawa za kulevya kutokana na maambukizi yake yanatokana na utumiaji wa dawa.

Alisema mwaka jana walikamata dawa tani 2.3 ambazo zingeingia nchini kungekuwa na kundi kubwa ambao wanatumia dawa hizo.
Mchambuzi Mkuu wa Mifumo ya Komputa wa Tume ya Taifa ya kudhibiti  Ukimwi (DCC),January Ntisi akizindua kitabu cha ripoti ya Bodi ya Kupambana na Dawa za Kulevya ya Umoja wa Mataifa,uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa idara ya habari- Maelezo,jijini Dar es salaam.Kushoni ni Afisa Mipango wa Umoja wa Mataifa,Immaculata Malyamkono-Nyoni na katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Kupambana na Watumiaji wa Madawa ya Kulevya,Very Kunambi.Picha na Emmanuel Massaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...