Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ally Kiba(katikati)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusiana na jinsi anavyojiandaa kuwapagawisha mashabiki wake katika Tamasha la Mwana Dar Live lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania na litakalofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam siku ya Pasaka.Wengine katika picha kushoto Msanii wa nyimbo za mchiriku Sueleman Jabiri”Msaga Sumu” na Kiongozi wa kikundi cha Warriors Damian Darada(kulia).
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kulia)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa kuwatambulisha wasanii wa muziki watakaotumbuiza katika Tamasha la Mwana Dar Live lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania na litakalofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam siku ya Pasaka.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Kiongozi wa kikundi cha Warriors Damian Darada, Mkurugenzi Mtendaji wa On Point Solution Bahati Singh ambao ni wakala wa kinywaji cha Vita Malt Nchini na Meneja Mkuu wa ukumbi wa Dar Live, Abdallah Mrisho.
Meneja Mkuu wa ukumbi wa Dar Live, Abdallah Mrisho(wapili toka kushoto)akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa kuwatambulisha wasanii wa muziki watakaotumbuiza katika Tamasha la Mwana Dar Live lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam siku ya Pasaka,kushoto kwake ni Mkurugenzi mtendaji wa On Point Solution Bahati Singh ambao ni wakala wa kinywaji cha Vita Malt Nchini na watatu toka kushoto ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu na Msanii wa nyimbo za mchiriku Sueleman Jabiri”Msaga Sumu”.
Baadhi ya wasanii watakaotumbuiza katika Tamasha la Mwana Dar Live lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam siku ya Pasaka wakionesha mshikamano kwa kushikana mikono pamoja na waandaaji na wadhamini kwa ajili ya kushiriki katika tamasha hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...