Kamati ya Bunge Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imetoa muda wa wiki mbili kwa Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) na Wakala wa Barabara (TANROAD) kutoa taarifa ya inayoeleza muda halisi wa kuanza kwa mabasi ya mradi huo katika kipindi cha mpito. 
 Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge, Bw. Hamis Kigwangala alitoa maelekezo hayo jana jijini Dar es Salaam wakati kamati yake ilipokuwa ikipokea taarifa ya utekelezaji wa maradi huo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia DART na TANROADS. “Kipindi cha mpito cha mradi huu kilikuwa kianze mwezi April mwaka huu lakini hadi sasa maandalizi yake bado hayakamilika,”alisema. 
Alisema kutokana na hali hiyo kamati imetoa siku 14 kuanzia sasa waandae taarifa inayoonyesha kukamilika kwa mandalizi hayo ikiwemo kusaini kwa mikataba na mtoa huduma na kuikabidhi taarifa hiyo. 
“Tunahitaji kuona mabasi ya kipindi cha mpito yanaanza kufanya kazi katika kipindi cha miezi miwili kuanzia sasa,” alisema. Alifafanua kwamba mradi huo ni muhimu kwa vile utaokoa Tshs 4.5 bilioni kwa siku zinazopotea katika jiji la Dar es Salaam kutokana na msongamano wa magari. 
Pia aliitaka TAMISEMI kwa kushirikiana na mamlaka nyingine kuhakikisha inawaondoa wafanyabiashara wanaofanya biashara zao katika miundombinu ya mradi huo. 
“Miundombinu hii imejengwa kwa gharama kubwa hivyo inapaswa kutunzwa na pia wananchi wanapaswa kuithamini” alisema. 
Alisisitiza kuwa Wakala uhakikishe mtoa huduma kipindi cha mpito anakuwa mzalendo na pia asizuiwe kuomba zabuni ya kuwa mtoa huduma mkuu muda utakapofika. 
Waziri, wa TAMISEMI, Mhe. Hawa Ghasia alisema serikali kwa upande wake itaendelea kutoa kipaumbe kwa wafanyabiashara wazawa kuendesha mradi huo. “Jambo zuri ni kwamba hata kamati ya bunge nayo inasisitiza kuwa wazawa wapewe kiupaumbele katika jambo hili,”alisema. 
Alisema serikali imepokea maelekezo yote yaliyotolewa na kamati ya bunge na wataenda kuyafanyia kazi dhamira ikiwa ni kuhakikisha mradi unaanza mara moja. 
Mtendaji Mkuu wa DART, Bi, Asteria Mlambo alisema mradi huo hadi sasa umetumia Tshs bilioni 413,836 na kusema kuwa kumekuwa na ongezeko la Tshs bilioni 122,841. 
“Benki ya Dunia inajiandaa kutoa mkopo wa pili wa fedha za ziada ambapo itatoa nusu na nusu nyingine inaombwa itolewe na serikali,” alisema. Alisema ongezeko hilo limetokana na mahitaji ya kujengwa kwa barabara za juu katika makutano ya Ubungo na kuongezeka kwa kima cha chini cha mishahara ya wafanyakazi wa ujenzi.
 Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya serikali za mitaa na tawala za mikoa (Tamisemi) Mh. Hamis Kigwangala (kushoto) akisikiliza maelezo ya Meneja Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka kutoka TANROADS Mhandisi Elibariki Mmari wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka, (kulia) ni Mtendaji Mkuu wa DART Asteria Mlambo (wa pili) ni Mhandisi Athuman Mfutakamba mbunge wa jimbo la Igalua na mjumbe wa kamati hiyo.
 Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya serikali za mitaa na tawala za mikoa (Tamisemi) Mh. Hamis Kigwangala (wa pili kulia) akimweleza jambo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI Hawa Ghasia wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa mabasi yaendayo haraka, (kulia) ni Mjumbe wa kamati hiyo Moses Machali (wa pili kushoto)  ni Naibu waziri TAMISEMI Kasim Majaliwa.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka ( DART) Asteria Mlambo (kulia) akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya serikali za mitaa na tawala za mikoa (Tamisemi) Mh. Hamis Kigwangala (wa pili kulia)  wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa mabasi yaendayo haraka, (wa pili kulia) ni Waziri wa nchi – TAMISEMI, Mh. Hawa Ghasia, (kulia) ni Mhandisi Athuman Mfutakamba mbunge wa jimbo la Igalua na mjumbe wa kamati hiyo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka ( DART) Asteria Mlambo (kushoto) akimweleza jambo Waziri wa nchi – TAMISEMI, Mh. Hawa Ghasia (katikati)   wakati kamati ya bunge ya tawala za mikoa na serikali za mitaa ( TAMISEMI) ilipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa mabasi yaendayo haraka, (kulia) ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh. Hamis Kigwangala.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...