Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa uwanja wa ndege mjini Dodoma mapema leo asubuhi na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo, Mh. Adam Kimbisa,tayari kwa kuanza ziara ya siku tisa, yenye lengo la kukagua, kuhimiza miradi ya maendeleo ya wananchi pamoja na kuangalia uhai wa chama, ambapo mara baada ya kuwasili amefanya mkutano wa ndani na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Wilaya ya Mpwapwa yenye majimbo mawili ya Uchaguzi.Kinana ametokea Mkoani Ruvuma mara baada ya kushiriki mazishi ya aliekuwa Mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi,Marehemu Kapteni John Komba aliyezikwa kijijini kwao Lituhi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa,Nape Nnauye akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh.Chiku Galawa mapema leo asubuhi mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege,tayari kwa kuanza ziara ya siku 9 mkoani humo,
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa,Mh.Addam Kimbisa akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Ujumbe wake pamoja na baadhi ya Wananchi (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili katika ofisi za CCM Wilaya ya Mpwapa mapema leo asubuhi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na baadhi ya Wanachama wa CCM waliofika mapema leo katika ofisi za CCM wilaya ya Mpwapwa kumpokea Ndugu Kinana na Ujumbe wake,ambapo anaanza rasmi ziara yake wilayani humu na vitongoji vyake.

PICHA NA MICHUZIJR-MPWAPWA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. OH! konoz ya mkuu iko vema kabisa...!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...