Mwakilishi wa Katibu Mkuu na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw.Elibariki Maleko(katikati) akizungumza kuukaribisha Ujumbe kutoka Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha nchini Nigeria (hawapo pichani) ulipokutana na Watendaji wa Wizara kwa ajili ya kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu Sera ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa. Ujumbe huo unaongozwa na Brigedia Generali Jimoh (wa pili kushoto) na upo nchini kwa ziara ya mafunzo. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Bw.James Lugaganya ( kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Bw. Innocent Shiyo (wa pili kulia) na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Bi.Maulidah Hassan.

Mwenyeji wa Ujumbe huo kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Brigedia Jenerali Mwemnjudi (mwenye nguo nyeupe) pamoja na Mwambata wa Jeshi katika Ubalozi wa Nigeria hapa nchini Brigedia Jenerali Erick Angaye wakimsikiliza Bw. Maleko (hayupo pichani).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera Nigeria kwa uchaguzi wa amani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...