Na Mwandishi Maalum, New York
Wakati hali  ya kisiasa na kiusalama ikiendelea kuwa ya sintofahamu Nchini Burundi, Katibu  Mkuu wa Umoja wa  Mataifa, Ban  Ki Moon (pichani), ameelezea kutiwa moyo na juhudi mbambali zinazolenga kurejesha hali ya amani na usalama nchi humo .
Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Katibu Mkuu,  siku ya Ijumaa hapa Umoja wa Mataifa,  imesema,  katibu Mkuu anatiwa  moyo na juhudi zinazofanywa na makundi mbalimbali  ya kikanda, ya kidini,  ya kijamii,  vyama vya siasa  pamoja na Mwakilishi Wake  Maalum  katika Eneo  la Maziwa Makuu katika kuhakikisha kwamba mgogoro  na sitofahamu iliyoikumba Burundi inatafutiwa ufumbuzi.
Wahusika wakuu ambao Ban Ki Moon ameelezea kutiwa moyo na juhudi zao za kuleta amani nchini Burundi ni  pamoja na Jumuiya ya   Afrika   Mashariki  (EAC) ambayo ipo chini ya uenyekiti wa Mhe. Rais   Jakaya Mrisho Kikwete,  Umoja wa   Afrika ( AU), Soko la  pamoja la Afrika  Mashariki na  Kusini mwa Afrika  ( COMESA),  Mkutano wa Kimataifa wa Eneo la Maziwa Makuu (  ICGLR) na  Mwakilishi wake Maalum katika eneo la  maziwa Makuu  Bw. Said Djinnit.
“ Katibu Mkuu  anawapongea washirika wote  wanaoshiriki mchakato huo pamoja na mafanikio yaliyofikiwa hadi sasa, hususani katika  kupunguza hali ya wasiwasi na sintofahamu na  kujenga mazingira ya  kufanyika kwa uchaguzi  huru, wa haki, jumuishi na wa amani.”  Inasomeka Taarifa ya katibu Mkuu
 Hata hiyo pamoja na kutiwa moyo na  kazi nzuri inayoendelea kufanyika,  Katibu Mkuu ameelezea  wasi wasi wake hali mbaya  ya kibinadamu inayowakabiri  wakimbizi kutoka  Burundi  ambao wamekimbilia nchi za jirani ikiwamo Tanzania.
Pamoja na wasiwasi huo Ban Ki  Moon  amezipongeza nchi jirani kwa  kutoa misaada ya kibinadamu ikiwa ni pamoja  na kuwahifadhi wakimbizi hao.  Huku akitoa wito kwa Serikali ya Burundi  kuandaa mazingira ya  kuwarejesha nchi humo raia wake waliokimbia machafuko.
Vile vile Katibu Mkuuu, amewahimiza wadau mbalimbali kuendelea na  majadiliano kwa lengo  la kufikia makubaliano ya jumla katika  maeneo yote ambayo  wameyaainisha. Huku akithibitisha utayari wa Umoja wa Mataifa  katika kuwasaidia  wananchi wa Burundi na   Kanda kwa ujumla katika  mchakato huu.
Taarifa kutoka Mashirika ya Kimataifa likiwamo la  wakimbizi, UNHCR zinazonyesha kwamba tangu mwezi Aprili mwaka huu, jumla ya wananchi 100,000 wa Burundi wakimbia nchi yao na kuvuka mipaka na kuingia katika nchi za Tanzania, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Wimbi hilo la wakimbizi, limesababisha  kuibuka kwa ugonjwa wa  kipindupindu katika kambi  iliyoko  Kigoma ugonjwa ambao umesabisha  vifo vya watu 37 kwa mujibu wa UNHCR  na kwamba  Serikali ya Tanzania imekwish kutangaza uwepo wa ugonjwa huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...