Mkurugenzi wa Bayport Financial Services, John Mbaga, pichani, akizungumza jambo katika uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo ya viwanja katika mradi wa Vikuruti, Kibaha, mkoani Pwani. Uzinduzi huo ulifanyika Ijumaa ya Mei 22, katika Hoteli ya Serena na kuhudhuriwa na watu mbalimbali, wakiwamo viongozi wa serikali. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaama

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, inayojihusisha na mikopo, imeanzisha huduma mpya ya kukopesha viwanja watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni za kawaida na wajasiriamali wa aina zote.

Kuanzishwa kwa huduma hiyo mpya kumetokana na taasisi hiyo kupania kuboresha maisha ya Watanzania, likiwamo kundi la wajasiriamali ambalo limeendelea kusahauliwa na kampuni nyingi kupewa mikopo.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, akizungumza katika uzinduzi huo, jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 25, 2015

    Ngula, you need to practice reading in Kiswahili more

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...