Mwenyekiti Mtendaji wa Michuzi Media Group (MMG) Ankal Muhidin Issa Michuzi (kulia) na Meneja
Maslahi na Sheria wa Kituo cha redio cha 93.7 E-Fm
Bw. Denis Ssebo wakipeana mikono baada
ya kusaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano
kwenye hafla fupi zilizofanyika Jumatano
Mei 6, 2015 kwenye ofisi za kituo hicho cha redio Mikocheni jijini Dar es
salaam.
Pamoja na mambo mengine MMG na Kituo
cha redio cha 93.7 E-FM kuanzia sasa watashirikiana katika mambo ya habari,
matangazo na shughuli zingine za kijamii ikiwa ni pamoja na michezo, muziki na
utamaduni.
“Hii ni siku ya kihistoria katika
tasnia ya habari nchini Tanzania kwa makubaliano haya ya kwanza ya aina yake ambapo
kituo chetu cha 93.7 E-FM kilicho mstari wa mbele kukuza tasnia za michezo, muziki na utamaduni wa
Tanzania na MMG inayoendesha na kuongoza katika tasnia ya habari mtandanoni nchini ya Michuzi Blog pamoja na Michuzi online TV
kukubaliana kufanya kazi pamoja.
“Hii ni baada ya kila upande kugundua kwamba
ina wapenzi lukuki ndani na nje ya Tanzania kuliko vyombo takriban vyote vya habari Tanzania, na pia kwa pamoja kuona haja ya
kuenzi na kukuza tasnia za michezo, muziki na utamaduni wa Tanzania ambavyo pamoja na
umuhimu wake vyombo vingi vya habari havijazipa tasnia hizo msukumo wa kutosha.
“Hivyo sisi kwa pamoja tumeamua
kuungana na kufanya mabadiliko makubwa kwenye kuendeleza tasnia za michezo,
muziki na utamaduni kwa nguvu zetu zote”, alisema Bw. Ssebo.
Kwa pande wake, Ankal, ambaye anaamini
katika vitendo zaidi ya kuongea, alisema MMG inayoendesha Michuzi Blog a.k.a Globu ya
Jamii, pamoja na Michuzi TV online, watafanya kile ambacho wengi hawafanyi ama
kama wanafanya inakuwa kijuu juu tu.
“93.7 E-FM radio station imedhihirisha
ndani ya mwaka mmoja tu kwamba michezo, utamaduni na jamii ya Tanzania vinaweza
kupendwa na kuthaminiwa na kila mtu ndani nan je ya Tanzania…
“Kwa kuwa Ubunifu, kujituma na juu ya
yote kuwapa wananchi kile roho zao zinapenda ni dira ya MMG na kituo hiki cha redio
kinachokuja juu kwa kasi ya ajabu na kustua, wadau wetu wakae mkao wa kula kila
siku kwani maneno hayavunji mfupa”alisema Ankal, ambaye blog yake pendwa kuliko
zote nchini ya Michuzi Blog mwaka huu inatimiza miaka 10 ya kuanzishwa kwake.
Kituo cha redio cha 93.7 E-FM kina mwaka mmoja tu toka kuanzishwa kwake lakini kimetokea kuwa kituo pendwa nchini Tanzania kwa kuenzi tasnia za michezo, muziki na utamaduni, wakati Globu ya Jamii inatajwa kuwa ndiyo Blog ya Kiswahili inayosomwa zaidi duniani.
Kituo cha redio cha 93.7 E-FM kina mwaka mmoja tu toka kuanzishwa kwake lakini kimetokea kuwa kituo pendwa nchini Tanzania kwa kuenzi tasnia za michezo, muziki na utamaduni, wakati Globu ya Jamii inatajwa kuwa ndiyo Blog ya Kiswahili inayosomwa zaidi duniani.
Natoa hongera sana kwenu kwa hatua hii mliyochukua. Ankal amekuwa mwalimu wangu katika ukuaji wangu kama mwanablogu. Namtakia yeye na washirika wake wapya mafanikio tele katika kuendeleza libeneke.
ReplyDeleteHongera sana MMG na 93.7 E- FM, tunataraji mengi zaidi kutoka kwa lijendari Ankal na magwiji wa tasnia ya utangazaji walojazana Efm habari ya mujini.
ReplyDeleteDaah Mithupu umechemka, hii post umeandika Friday May 8!!!!!!????? Hatujafika Ijumaa kaka au upo Sydney?
ReplyDelete