Na Avila kakingo,Globu ya Jamii.
CHAMA cha wafugaji Tanzania (CCWT),kimewataka
wafugaji wote nchini kufanya shughuli zao kwa kufuata sheria, pia hawataki
kuona wafugaji wakifanya uonevu wa aina yoyote kwa watu wengine.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa chama cha Wafugaji Tanzania
(CCWT),Magembe Makoye wakati akizungumza na wandishi wa habari katika ukumbi wa
Habari MAELEZO leo jijini Da es Salaam.
Makoye Amesema kuwa wafugaji watambue kuwa kunakutegemeana na watu
wengine katika kuendesha shughuli zao bila kuathiri watu wengine
katika jamii.
Pia Makoye amesisitiza kuwa chama cha wafugaji Tanzania hakitavumilia
kuona wafugaji wanakuwa chanzo cha migogoro katika jamii,aidha chama hicho kimetoa wito kwa wafugaji wote Tanzania
kujihadhali na watu wanaopita kwao na kujitambulisha
kuwa wao ni viongozi wa chama cha wafugaji Tanzania.
Chama hicho kimeitaka Serikali itenge ardhi
kwa ajili ya wafugaji ili kuepuka mwingiliano uliopo sasa wa watu
kutokujua mipaka yao na hatimaye kusababisha mapigano na uhasama miongoni
mwa makundi hayo,
Katibu Mkuu wa Chama cha Wafugaji Tanzania,Magembe Makoye akizungumza na
wandishi wa habari kushusiana na wafugaji kufanya shughuli zao kwa
kufuata sheria za nchi katika ukumbi wa Habari MAELEZO leo jijini Dar es Salaam
kulia ni Mkurugezi Msaidizi wa Idara ya HABARI MAELEZO Tiganya Vincent .
Baadhi ya waandishi wa habari (PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA
JAMII)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...