Mkurugenzi Msaidizi wa Upimaji na Ramani vijijini wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Huruma Lugalla (kushoto) akitoa maelekezo kwa wataalam wa Upimaji na Ramani wa wizara hiyo wakati wa uhakiki wa moja ya ramani ya eneo linalopaswa kuwa la makazi ya watu na taasisi nje kidogo ya mji wa Chalinze, Bagamoyo mkoani Pwani iliyopimwa na Kampuni ya Intergrated Property Consultancy and Services (IPCS) ya Morogoro na kubainika kuwa chini ya kiwango.
Wataalam wa Upimaji na Ramani wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakifanya uhakiki wa moja ya ramani ya eneo linalopaswa kuwa la makazi ya watu na taasisi nje kidogo ya mji wa Chalinze, Bagamoyo mkoani Pwani lililopimwa chini ya kiwango. Katikati (aliyesimama) ni Bw. Bernard Malugu, Mkurugenzi wa Kampuni ya Intergrated Property Consultancy and Services (IPCS) ya Morogoro iliyoifanya kazi hiyo chini ya kiwango.
Mkurugenzi Msaidizi wa Upimaji na Ramani vijijini wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Huruma Lugalla (kushoto) akifuatilia moja ya eneo ambalo lilitakiwa kuwa na alama ya mpaka ambalo halikuwa na alama yoyote wakati wa uhakiki wa moja ya ramani ya eneo linalopaswa kuwa la makazi ya watu na taasisi nje kidogo ya mji wa Chalinze, Bagamoyo mkoani Pwani iliyopimwa na Kampuni ya Intergrated Property Consultancy and Services (IPCS) ya Morogoro ambayo ilibainika kuwa chini ya kiwango. Kulia ni Bw.Allex Kachoka Mpima Ardhi wa wizara hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...