Bi. Bernadette Mathias ambaye kwa kushirikiana na mpiga piano mumewe Profesa Philip Mathias wakitumbuiza kwa wimbo wa "Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo wote" kwa ufasaha na kusisimua waliohudhuria sherehe za Rais Jakaya Mrisho Kikwete kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Chuo Kikuu cha Newcastle nchini Australia Julai 29, 2015. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 30, 2015

    Wow she killed it..........

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 30, 2015

    Asante sana Bernadette kwa kutuimbia wimbo Tanzania.
    Unanikumbusha nyumbani wakati nasoma. Sijui kama mashuleni bado wanafundisha nyimbo kama hizi

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 30, 2015

    Safi, sasa hii ilikuwa wapi jamani?

    habari haijakamilika

    Anon

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 30, 2015

    Wimbo huu "Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo wote -----"umeimbwa vizuri sana na mama huyu wa Australia na hiyo band ya muziki kuliko hata ambavyo baadhi yetu Watanzania wazalendo tungeweza kuuimba. Swali ni je, wangapi huo wimbo wangeweza au wanaweza kuuimba kwa ufasaha kama mama huyo wa Ausralia? Amempa heshima sana Rais wetu.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 31, 2015

    Wimbo huu uko kama wimbo wa huzuni. Wimbo wa "sisi tunataka kuwasha mwenge" ndiyo tunaopaswa kuuimba zaidi. Pia wimbo wa " tazama ramani" nao ni mzuri, na unasisimua kuliko huo alioimba huyo mama.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 31, 2015

    Tanzania Tanzania siku zote ni Wimbo mzuri. Bernadette ameimba vizuri na kutukumbusha kuwa tuna wimbo wetu. Mimi najiuliza nini kifanyike ili tung'amue kwamba huu ndito wimbo wa taifa. Yes kuna verses za kuongeza pamoja na chorus. Mungu ibariki tune si ya asili yetu tuachane nao.

    ReplyDelete
  7. Ningekuwa JK ningempa huyu Trip ya kuja TZ kuiona nchi aliyoiimba na kuona vivuitio vya utalii. Inawezekana kaimba hata TZ kwenyewe hajafika.

    ReplyDelete
  8. DADA KAUA KABISA......YAANI MPAKA KACHOZI KAMENIBUBUJIKA...NAKUMBUKA NIMECHELEWA SHULE NIMECHELEWA NAMBA WATU WAPO MSTALINI NATAKA KUINGIA TU KAMWIMBO KANAANZA BASI NAZUGA MPAKA NAKAA KWENYE LINE NAKUANZA KUUIMBA KWA HISIA ..........HAKIKA TANZANIA HII NI MAMA TUMTUNZE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...