Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva (katikati) Akizungumza katika Uzinduzi Huo Akiwa na   Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya EAG Group LTD Imani Kajula (Kushoto) Pamoja na Meneja Uendeshaji wa Premier Mobile Solutions, Bi Lulu Ramole.
Simba Sports Club kwa kushirikiana na Kampuni ya Tigo Tanzania zimezindua huduma ya ujumbe mfupi ijulikanayo kama ‘SIMBA NEWS’, ambayo lengo lake nikuwapatia wateja wa Tigo taarifa zinazoihusu klabu ya Simba popote walipo nchini.
Huduma hii mpya inajulikana kama ‘SIMBA NEWS’. Njia hii ni rahisi na yenye ufanisi yenye kuifanya dunia ijulikane kwa wateja wake.

 “Pamoja na kasi yaukuaji wa Tehama, Tigo inaelewa umuhimu wakutoa taarifa kwa wateja wake, ndiyo maana leo, tunajisikia fahari kuzindua huduma hii iliyotengenezwa vizuri ya SIMBA NEWS nawashirika wetu wa klabu ya SIMBA, EAG Group LTD pamoja na Premier Mobile Solutions (PMS), ilikuendelea kuwapa wateja wetu taarifa zinazohusu masuala ya sasa huku wakifurahia habari mpya zinazohusu klabu,”alisema meneja wa mawasiliano ya kibiashara Jacqueline Nnunduma.
Lengo letu si tu kuwapatia wateja wetu taarifa kiurahisi zaidi, lakini pia kuwapatia taarifa hizo kwa wakati na zenye uhakika kutoka vyanzo vya michezo vyenye kuaminika,” aliongeza Nnunduma.
Akizungumza kwa niaba ya Klabu ya Simba,Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva alisema, “Tunaamini ubunifu huu bila shaka utawawezesha mashabiki wote wa Simba na wa soka kwa ujumla ambao pia ni wateja wa Tigo kupata habari mbalimbali za klabu ya Simba kupitia simu zao za mkononi”.
Tunawahimiza mashabiki wetu kujiunga na huduma hii kupitia Tigo ili waweze kupata nakufurahia habari mbalimbali kutoka klabu ya Simba. Aliendelea Aveva.
Akiongea katika tukio hilo Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya EAG Group LTD Imani Kajula ambao ni washauri na watekelezaji wa shughuli za kibiashara na masoko katika klabu ya Simba, alisema “Tunatarajia kuendelea kuwapatia mashabiki wa Simba huduma za kisasa kwa kutumia teknolojia zisizokuwa na usumbufu wa aina yeyote kupitia wadau wanaoaminika ndani ya Tanzania”
Kwa upande wake Meneja Uendeshaji wa Premier Mobile Solutions, Bi Lulu Ramole alisema kuwa huduma hii imetengenezwa ili kuwawezesha wateja kupata habari za papo kwa papo naaliongeza kuwa huduma ipo katika mfumo wa vifurushi vya Combo / BUNDLE PACK ambapo wateja wa Tigo watakuwa wakilipia mara moja kwa siku na kupokea kiwango cha chini cha habari nne (04) na habari mpya za kila siku zina zohusu klabu ya Simba.
Huduma pia itamruhusu mteja aliyejiunga kujitoa kwenye huduma hii wakati wowote akitaka bila vikwazo vyovyote na pia kwenye huduma hii kutakuwepo na neon kuu “MSAADA”kwa ajili ya kusaidia juu ya maswali mbalimbali ya nayo ulizwa mara kwa mara na wateja wakati wakifurahia huduma.
Ili kujiunga na huduma hizi unatakiwa kutuma neon kuu SIMBA kwenda 15460. Utakapo jiunga tu mteja atapokea habari kutokana na neon analolituma kila siku na atatozwa kiasi cha shilingi za kitanzania 150 kwa siku. Na ili kujitoa kwenye huduma mteja atahitaji kutuma neno ONDOA SIMBA kwenda 15,460.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...