Zahara Muhidin Michuzi akiwa nje ya ukumbi wa uchaguzi mapema leo.
Na Mkala Fundikira wa 
TBN kanda ya Magharibi
Leo hii mchana binti ya mpiga picha na blogger maarufu nchini Muhidin Issa Michuzi Bi Zahara Michuzi alishindwa kupata kura za kutosha kumwezesha kushinda nafasi ya ubunge wa vijana kupitia tiketi ya CCM mkoa wa Tabora baada ya msanii wa filamu Bi Irene Uwoya kupata kura 34 kati ya 39 zilizopigwa.

Zahara ambaye ni mhitimu wa shahada ya uchumi toka chuo kikuu cha UDOM aliyakubali matokeo hayo bila kinyongo  na kusema :
"Napenda kuwashukuru wagombea wenzangu na wajumbe wote. Pamoja na kura mlizonipigia hazikutosha leo lakini nitabaki na azma yangu ya kuwatumikia wana Tabora" wajumbe walimshangilia sana na kumpongeza kwa ukomavu wa kisiasa aliouonesha kwani mgombea  mwenzie Mariam Shamte alisusia na kuondoka ukumbini. 
Mariam alimteua nduguye Hapsa kumwakilisha ktk uhesabuji kura hizo ambazo yeye Mariam alipata kura 3. Hakuingia ukumbini katika usomwaji wa matokeo.

Awali mgeni rasmi wa mkitano huo mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Bw Hassan Wakasuvi aliwaeleza wajumbe kuwa Obama alizaliwa na baba raia wa Kenya na mama Mmarekani lakini leo hii anaiongoza Marekani, hivyo wasione ajabu kama pana mgombea asiyetokea Tabora kiasilia. 
Bila shaka alikuwa akimzungumzia Irene Uwoya ambaye kabla ya uchaguzi wakazi wengi wa Tabora walielekea kutomkubali kwa kusema kwa nini CCM ituletee mgombea toka Arusha, Moshi au Dar es Salaam, na kwa nini Irene asigombee Dar anapoishi au Kwao kaskazini? kwani Tabora hakuna vijana wenye uwezo wa kugombea? 
Waliendelea kuhoji kuwa ni vipi Irene atayajua matatizo ya vijana wa Tabora ambao hawajui wala hana uelewa na mkoa huo? 
Lakini hayawi hayawi hatimaye yamekuwa kwa Irene ameibuka mshindi katika kinyang'anyiro hicho. 
Kama maneno ya Mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Tabora yalifanya kazi kusababisha Irene Uwoya achaguliwe kwa kishindo mimi na wewe hatujui.
Zahara Michuzi akiwa na wagombea wenzie Mariam katikati na Irene kulia
Irene Uwoya mcheza sinema maarufu nchini alishinda uchaguzi huo kwa kura 34 kati ya 39 zilizopigwa.
Mariam Shamte alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 3
Zahara Muhidin Michuzi alishika nafasi ya 3 kwa kupata kura 2 katika kura 39 zilizopigwa.
Bi Mariam Amir katibu wa UVCCM mkoa wa Tabora akisoma tamko la kuunga mkono na kupongeza kuchaguliwa Bw John Magufuli kuwa mgombea urais wa Jamhuhuri ya muungano wa Tanzania.
Katibu mkuu wa CCM mkoa wa Tabora Bibi Janeth Kayanda akisalimia wajumbe leo hii mapema.
Mwenyekiti mstaafu UVCCM wilaya ya Tabora mjini Nassor Wazambi akifuatilia mchakato.
Wagombea wakiwasalimia wajumbe wa mkutano maalumu leo mapema.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Tabora Bw Seif Gulama (Kazuge) akitoa yake machache.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Mzee Hassan Wakasuvi akihutubia mkutano huo.
Sunday Kabaye akiwa amebeba sanduku la kura mara baada ya kura hizo kuhesabiwa nyuma akifuatiwa na Irene Uwoya na Zahara Michuzi.
Irene Uwoya akitokwa machozi kabla ya kutangazwa mshindi
Kada wa CCM Jaha Kaducha kushoto akiwa na Mwalimu Nassoro Wazambi.
Msimamizi wa uchaguzi Bw Mwambeleko akisoma matokeo ya uchguzi huo leo mchana mijini Tabora
Team Irene wakifuatilia mchakato

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. The mdudu, mjomba Michuzi tusikubali kabisa na haya matokeo lazima tukate rufaa kwa sababu wamejifunga wenyewe eti wanachi wengi walikua wanahoji kwanini tuletewe mtu ambae sio mzaliwa wa TABORA? sasa tuje kwenye ukweli kama wanachi walishasema hatumtaki mtu ambae sio mzaliwa wa TABORA sasa ni nani aliepiga hizi kula na zimepigwa kwa faida ya NANI? Huu mdada Uwoza or sorry UWONYA or sorry Uwoya lazima limetoa NGONO kama rushwa ili ashinde nahisi ngono kapewa huyo anaesema Obama ni mkenya lakini sasa ni Rais wa Marekani yaani kuonyesha tayari likibumbuluka atayasema haya maneno mimi the The mdudu nipo huku Uingereza imeniuuma sana hii kitu mjomba naomba kawaone Takukulu ili wachunguze kwa kina coz haiingii AKILINI bint yetu msomi na mtabora halisi kisha wamkate mchana kweupe wadau wote wa mjomba Michuzi chonde chonde tufungeni kibwebwe mpaka binti wa Mjomba Michuzi kieleweke shime shime WADAU WOTE.

    ReplyDelete
  2. aliye nyuma ya Irene inaonekana ana misuli sana


    ReplyDelete
  3. Dada yetu hamia Ukawa kama akina Lowasa

    ReplyDelete
  4. Hapo ccm ndipo inapoipeleka nchi .., duh!
    Kijana mwemye elimu., heshima , muono wa kijamii, ukaribu na wana mji, eti kashindwa!!??... Hahahaha.
    Huyo uwoya nani asijyemjua kwa hayo zahara aliyo nayo? It's pain.
    Mdau jp.

    ReplyDelete
  5. Duh! Ndo maana hii kitu inaitwa SI HASA. Maajabu hataisha hapa duniani lkn Uwoya kaiona fursa na kaitumia. Hivi hiyo ndo mwisho (tayari kawa mbunge) ama kuna hatua nyingine?

    Kuna haja ya kuangalia hii kitu hao watu ni wachache sana kumchagua mwakilishi wa mkoa mzima jamai. Ni rahisi kuwanunua wote. Uwanja upanuliwe ili mwakilishi awe mwakilishi kweli.

    Hiyo "comment ya kwanza ya Mdudu ungeipotezea ina chembe za ukweli lkn ni ngumu kudhibitisha jamani.

    Observer

    ReplyDelete
  6. Ina mana kapata MBILI tuuuuu!

    Nakubaliana kwa asilimia zote maoni ya mdau no. 4 hapo juu. Binafsi nashindwa kushawishika na kukubaliana na matokeo hayo, kuna dhulma hapo. Ni nini khasa kinachoangaliwa zaidi katika hizi chaguzi zetu kwa jumla, umaarufu au.....??!!

    ReplyDelete
  7. Wakati ujao anza mapema kampeni za chini chini, ikifika wakati wa uchaguzi watakuwa wameisha kujua, Michuzi muwezeshe kuanzisha NGO ya vijana iwe ikitoa miongozo kuhusu maendeleo ya vijana na kukusanya fedha kwa ajili hii, lengo lake la uongozi litatimia katika kuinua vijana, kuna pengo linalotakiwa kuzibwa katika kuhamasisha maendeleo, uwajibikaji na ujasiriamali katika nchi yetu.

    ReplyDelete
  8. THIS IS INSANE! TANZANIA ISIPOANGALIA ITAKUWA NA MAMBUMBUMBU BUNGENI.. AIBU AIBU AIBU HUYU MCHEZA SINEMA AMBAE HANA ELIMU KUSHINDA NA WALE WENYE ELIMU NA UPEO WA KUFANYA KAZI WAKAACHWA NYUMA. HILI WIMBI LA WANAOJIITA "CELEBRITIES" KUINGILIA SIASA LAZIMA LIKOMESHWE LA SIVYO NCHI ITAONGOZWA NA KINA VIHIYO NA KUISHIA KUIUZA KWA WAGENI. ANKAL NAJUA NIMEKUKWAZA KWA UJUMBE WANGU LAKINI INABIDI NIONGEE KUTOKA ROHONI. TAFADHALI PEPERUSHA HUU UJUMBE.

    ReplyDelete
  9. Inatia kinyaa sana. Vihiyo wanazidi ku-take over bunge. Bure kabisa.

    Rutagwerera.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...