Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akifafanua jambo kwa umakini mbele ya waandishi wa habari  kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. 
  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. 

 Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.

 MGOMBEA mteule wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Pombe Magufuli, leo Jumanne Agosti 4, 2015  atawasili Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kuchukua fomu ya kuomba kugombea Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba Mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema, msafara wa Dk. Magufuli  kwenda kuchukua fomu hiyo, utaanza saa tano asubuhi ukitokea Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.
Nape amesema, msafara ambao utaambatana na shamrashamra za aina yake, utapita katika Barabara za Morogoro, Bibi Titi Mohammed na Ohio kabla ya kufika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi zilizopo Posta House, karibu na makao Makuu ya Jeshila Polisi.
Amesema, Dk. Magufuli ambaye ataambatana na Mgombeamwenza wake, Mhe. Samia Suluhu, mbali na makada, wapenzi na wanachama wa CCM,atasindikizwa na viongozi mbaimbali wakiwemo, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Dk. Magufuli alichaguliwa na Mkutano  Mku wa CCM uliofanyika Oktoba 11, 2015, mjini Dodoma, baada ya kuwashinda wagombea wenzake, Dk. Asha-Rose Migiro na Balozi Amina Salum Ally. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Tembo dume.......kachukue tingatinga lisafishe na kujenga nchi yetu ila nakuomba sana Jembe letu najua utashinda kwa kishindo Mr Tembo dume naona mbali sana kimaendeleo JIJI la DAR lazima lipatiwe waziri pekee tu wakuliangalia hilo city na aligeuze liwe mfano Africa nzima. Na serikali pia ihamie Dodoma na kwa utendaji wako ulitukuka naamini utanielewa kila la heri JEMBE la watanzania anaebisha asage chupa kisha ameze

    ReplyDelete
  2. Jumanne tarehe 3 August!

    ReplyDelete
  3. KWA KWELI MHE. NAPE UMEFANYA NA UNAENDELEA KUFANYA KAZI NZUURI SANA KWA CHAMA CHETU. UNASTAHILI PONGEZI NENE HASWAAAA

    ReplyDelete
  4. mh,JP endapo ukishinda wakumbuke askari police kimasirahi na mazingira yao ujumla

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...