ASILIMIA 46 ya wananchi wameripoti kuwa sera ndio kigezo muhimu watakachokitumia kumchagua Rais. Vigezo vingine vilivyotajwa na wananchi wengi ni uadilifu na maadili (17%). Hakuna mtu hata mmoja aliyetaja dini au utajiri kama kigezo muhimu cha kumchagua Rais na kigezo cha umri kilitajwa na asilimia moja tu ya wananchi.

Matokeo haya yametolewa na Twaweza kwenye muhtasari wa utafiti wenye jina la Je, Wanajua? Takwimu kuhusu uelewa wa wapiga kura. Muhtasari umetokana na Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaofanyika mara kwa mara kwa njia ya simu za mkononi. Matokeo yametokana na takwimu zilizokusanywa kwa wahojiwa 1,335 kutoka Tanzania Bara (Zanzibar haikuhusishwa) kati ya tarehe 12 na 26 mwezi Juni 2015.

Aidha, wananchi wanaamini kuwa uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 utakuwa huru na wa haki - asilimia 82 wanaamini kwamba maamuzi yao yataheshimiwa. Hata hivyo, asilimia 18 wanafikiri kuwa viongozi walio madarakani watavunja sheria ili washinde. 

Asilimia 65 ya wananchi wanaamini kwamba mgombea mwenye sera nzuri atamshinda yule mwenye pesa nyingi. 

Katika suala la vyombo vya habari, asilimia 76 ya wananchi wanaamini kwamba vyombo hivyo vitaripoti kwa usahihi masuala yanayohusu uchaguzi mkuu, wakati asilimia 24 wanafikiri kuwa vyombo vya habari vitakuwa na upendeleo kwa sababu ya motisha ya fedha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...