RPC wa Mkoa wa Dodoma SACP. David A. Misime akiongea na waandishi wa Habari leo akitoa tahadhari juu ya matapeli wanaowadanganya na kuwatapeli wastaafu. LAPF kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma imefanikiwa kumkamata mtu mmoja na kumfikisha Mahakamani baada ya kujifanya ni mtumishi wa TAMISEMI, LAPF na OFISI YA KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA na kufanikiwa kuwaibiwa fedha kwa njia ya mtandao wastaafu kutoka katika mikoa mbalimbali.
   Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama wa LAPF Bw. Valerian Mablangeti akitoa ufafanuzi katika mkutano huo na waandishi wa habari.
Baadhi ya washiriki.
MFUKO WA PENSHENI WA LAPF
  
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 02.09.2015
          MFUKO wa Pensheni wa LAPF unapenda kutoa kutoa tahadhari hasa kwa Wastaafu au wanaotarajia kustaafu, Idara, Wizara zote zinazoshughulika na wastaafu, Wakurugenzi wa Manispaa na Halmashauri kujihadhari na watu wanaowapigia simu na kujitambulisha kuwa wao ni watumishi wa Mashirika ya Hifadhi za Jamii na Idara zingine za Serikali na kwamba wanashughulika na mafao ya wastaafu.

          LAPF inatoa tahadhari hiyo kwa sababu kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma tumefanikiwa kumkamata mtu mmoja kwa jina la DAVID MAGESA MAKALI @ PETER MABULA na kumfikisha Mahakamani baada ya kujifanya ni mtumishi wa TAMISEMI, LAPF na OFISI YA KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA na kufanikiwa kuwaibiwa fedha kwa njia ya mtandao wastaafu kutoka katika mikoa mbalimbali.

          Wanachofanya watu hao wanapiga simu Idara mbalimbali na kujifanya wapo TAMISEMI au Wizara nyingine na kuwataka wawatumie orodha ya wastaafu wa mwaka fulani pamoja na namba zao za simu. Inaonyeha kwa njia hiyo wameweza kupata orodha ya wastaafu takriban kutoka katika Mikoa 15 hususan kutoka Idara ya afya. 

Wakishapata orodha ya majina ya wastaafu na namba zao za simu humpigia mstaafu na kujitambulisha anatokea Wizarani na anashughulikia wastaafu ambao inaonekana walipunjwa kwenye mafao yao na inaonyesha naye amepunjwa kiasi cha milioni fulani. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...