Happy Limwamwa (9-10) Pichani.
Happy Limwamwa 9-10 (kushoto) akizungumza kwa uchungu kwa Msaidizi wa Kisheria Geophrey Kaduma, (wapili kulia) kwa manyanyaso aliyokuwa akiyapata toka kwa mama aliyekuwa amemtowa kwao Wilaya ya Mbinga Mkoa wa Ruvuma, kwa malengo ya kufanya kazi za ndani, ndipo alipokutana na kichapo toka kwa mama huyo na mume wake na kumfanya akimbiye na kuishi mitaani.
Happy ambaye ameokotwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bryceson Mgaya wa Mtaa wa Kambarage Kata ya Njombe Mjini Wilaya ya Njombe Mkoa wa Njombe, Pamoja na Mwenyekiti huyo kutowa taarifa katika kituo cha Polisi na kumtembeza katika mitaa tofauti alipokuwa akifanya kazi zaidi ya wiki 3 bado juhudi yoyote haijazaa matunda kwa mtoto huyo kurudishwa kwao, kwa yoyote anaye weza kumfaham mtoto huyo awasiliane na Mwenyekiti huyo wa Mtaa, 0766336403, Mwenyekiti wa Kituo cha Sheria Geophrey Kaduma, 0759601915-o655601915. wapili kushoto ni Katibu wa Kituo cha Msaidizi wa Kisheria Magy Mtalla na wakwanza kulia ni mke wa mwenyekiti wa Mtaa wa Kambarage Matha Maiseli (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Katibu wa Kituo cha Msaidizi wa Kisheria Magy Mtalla, akizungumza na mtoto huyo Happy Limwamwa 9-10
Happy Limwamwa 9-10 akiwa katika picha
Si vizuri kufanyisha kazi watoto wafdogo kama hao. Kumwachia mtoo kama huyu alee watoto wako ukizingatia atakaa nao muda mrefu kuliko wewe hakuwasaidii wala kuwaongezea watoto bali ni kuwaacha bila mlezi.
ReplyDelete