FAMILIA ya marehemu mzee Japhet Mbaga, wa Dar es Salaam kwa masikitiko makubwa inatangaza vifo vya kaka zao wapendwa, MICHAEL NA JOHN JAPHET MBAGA, vilivyotokea hapa Dar es slaam  siku ya Jumapili na Jumatatu zilizopita.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam, siku ya Alhamisi tarehe 3 Septemba, 2015 saa 10.00 jioni. 

Ratiba ya kutoa heshima za mwisho itafanyika siku hiyo hiyo, saa 7.00 mchana nyumbani kwa Mary Rusimbi (Mkurugenzi Mkuu, WOMEN FUND TANZANIA) eneo la Tabata - shule, nyumba za TAZARA.

 Baadaye saa 9.00 Ibada ya kuwaaga wapendwa wetu itafanyika Kanisa la KKKT Kijitonyama.

Marehemu MICHAEL NA JOHN JAPHET MBAGA ni kaka wa MARY RUSIMBI, HILLARY MBAGA, ROSE MSHANA (ROZELLA) NA STELLA MBAGA.


"Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake na lihimidiwe."
AMINA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...