Na Joachim Mushi, Dodoma.
MGOMBEA mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu amesema Serikali itakayoundwa na chama hicho endapo itashika dola katika Uchaguzi mkuu wa Oktoba, 2015 itahakikisha inapima ardhi yote ya vijiji pamoja na kuainisha mipaka ili kukomesha migogoro ya ardhi. 

 Bi. Suluhu ametoa kauli hiyo alipokuwa akinadi ilaya ya CCM katika Majimbo mawili tofauti ya Kongwa na Chilonwa Mkoa wa Dodoma ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kufanya kampeni kuwashawishi Watanzania waweze kuipa ridhaa tena Chama Cha Mapinduzi ili kiunde Serikali na kuwatyumikia wananchi.

 Mgombea huyo mwenza wa urais akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Chilonwa Kijiji cha Nzali alisema Serikali ya CCM kwa kushirikiana na halmashauri itaipima ardha ya vijiji na kuweka mipata hasa maeneo sugu ya migogoro kama Kongwa na Kiteto ili kuzuia migogoro na mapigano kwa jamii hizo mbili.Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akipokea kadi kutoka kwa wanachama wa CHADEMA waliojiunga na CCM baada ya kukihama chama hicho. Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akiwa amepokea kadi kutoka kwa wanachama wa CHADEMA waliojiunga na CCM baada ya kukihama chama hicho. Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu. Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu.
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akipokea kadi kutoka kwa wanachama wa CHADEMA waliojiunga na CCM baada ya kukihama chama hicho. Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akipokea kadi kutoka kwa wanachama wa CHADEMA waliojiunga na CCM baada ya kukihama chama hicho.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...