Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai  Bw.Diwani Athumani (CP) akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo katika picha leo jijini Dar es Salaam kuhusu uchunguzi wa sakata la watuhumiwa wa wizi wa makontena 329.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Bw.Diwani Athumani (CP) alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu uchunguzi wa watuhumiwa wa wizi wa makontena kwa Mamlaka ya Bandari na Mamlaka ya Mapato Tanzania.

Na Nyakongo Manyama-Maelezo
KUFUATIA agizo laWaziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa la kuwataka watuhumiwa wa wizi wa makontena 329 katika bandari ya Dar es salaam kuchukuliwa hatua na Jeshi la Polisi, tayari Jeshi hilo limewashikilia watuhumiwa kumi na mbili wanaohusika na wizi huo. 

Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (CP) Diwani Athumani amesema kuwa, uchunguzi unaofanywa na wataalamu waliobobea katika makosa ya uhalifu wa kifedha umeweza kuwabaini watu kumi na mbili ambao wamehusika na wizi huo.
“Kati ya watuhumiwa hao kumi na mbili, watano wanashikiliwa na Jeshi la Polisi na saba bado wapo katika upepelezi na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani,” alisema Kamanda Athumani.


Wanaoshikiliwa kutokana na tuhuma mbalimbali ni Kamishna wa Idara ya Forodha na Ushuru TRA Bw. Tiagi Masamaki, Meneja Kitengo cha Huduma za Ushuru na  Habibu Mponezia, Msimamizi Mkuu wa Kitengo cha Ushuru wa Forodha.
Watuhumiwa wengine ni pamoja na Bi. Eliaichi Mrema, Msimamizi Kitengo cha Mawasiliano ya Kompyuta Bw. Haroun Mpande na Mchambuzi Mwandamizi wa Masuala ya Biashara Bw. Hamis Omary.


Aidha Kamanda Athumani amewaomba wananchi wenye taarifa za ubadhilifu wa mali za Umma kuendelea kulisaidia Jeshi la Polisi katika kutekeleza majukumu yake. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...