Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupambana na vitendo vya ukeketaji yamefanyika Mjini Dodoma, huku Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh Ummy Mwalimu akiwa mgeni rasmi. 

Maadhimisho hayo yalianza kwa maandamano yaliyoanzia viwanja vya Nyerere Square mpaka ukumbi wa Hazina Ndogo ambapo, Mh Ummy alitoa Tamko la msimamo wa serikali kuhusu ukatili wa ukeketaji na mipango ya Serikali ya awamu ya Tano kukabili ukiukwaji wa haki kutokana na vitendo hivi. 

ikiwemo mpango wa serikali kutunga na kuzifanyia marekebisho sheria kandamizi ili kuleta usawa wa jinsia. sheria hizo ni pamoja na sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 ya mwaka 2001, kifungu cha 158 (1) (a) na sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009ambayo inazuia ukeketaji kwa mtoto wa kike.

Maadhimisho haya yaniandaliwa na Children's diginity forum pamoja na shirika la kimataifa la UNFPA pamoja na serikali.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...