Mheshimiwa Ummy Ally Mwalimu (Mb.) Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto leo alikuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kupinga Ukeketaji Duniani yanayofanyika tarehe 5 Februari kila mwaka. Maadhimisho hayo kwa Mkoa wa Dodoma yalifanyika katika Ukumbi wa Hazina Dodoma, kwa kuratibiwa na Mtandao wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanayopinga Ukeketaji Tanzania.
Wakati wa maadhimisho hayo Mhe Waziri Ummy Mwalimu alieleza kuwa Kwa mujibu wa Takwimu za Demografia na Afya Tanzania (Tanzania Demographic and Health Survey - TDHS 2010) asilimia 15  ya wanawake Tanzania wamefanyiwa Ukeketaji. Ukeketaji ni ukatili dhidi ya watoto wa kike na wanawake. Na ni kosa la jinai. Madhara ya ukeketaji ni pamoja na vifo, vilema na maradhi kama fistula na mengineyo.

Alieleza kuwa Serikali itaendelea kukemea na kupambana na vitendo hivi katika jamii zetu. Na itaongeza jitihada za kutoa elimu kwa jamii sambamba na kuwachukulia hatua wote wanaojihusisha na vitendo hivi.

Mhe Waziri Ummy Mwalimu aliwataka Maafisa Maendeleo ya Jamii katika Mikoa, Wilaya na Kata kuongeza nguvu ktk kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa lengo la kuhakikisha wazazi/walezi, mangariba na wote wanaojihusisha na vitendo vya Ukeketaji wanafikishwa ktk vyombo vya dola ili sheria ichukue mkondo wake.

Aidha, alitoa wito kwa kila mwananchi kushiriki katika mapambano haya hasa katika kutoa taarifa na ushahidi Mahakamani.
Mheshimiwa Ummy Ally Mwalimu (Mb.) Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (mstari wa mbele katikati), Mkuu wa wilaya ya Dodoma  Dkt. Jasmine Tisekwa ( Kulia) na Muwakilishi wa UNFPA, Bi Christine Mwanukuzi ( Kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa Mtandao wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanayopinga Ukeketaji Tanzania, wakati wa maadhimisho ya Siku ya kupinga ukeketaji kwa 
Mheshimiwa Ummy Ally Mwalimu (Mb.) Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akipokea maandamano ya wadau mbalimbali wa Maendeleo ya Mtoto katika viwanja vya ofisi za Hazina Dodoma wakati wa maadhimisho ya Siku ya kupinga ukeketaji kwa wanawake na watoto wa kike.wanawake na watoto wa kike.

Mheshimiwa Ummy Ally Mwalimu (Mb.) Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akihutubia wadau mbalimbali wa Maendeleo ya Mtoto, wakati wa maadhimisho ya Siku ya kupinga ukeketaji kwa wanawake na watoto wa kike.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...