Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saady Kawemba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Msemaji wa Timu ya Azam FC, Jafari Iddy.

Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii..
UONGOZI wa Azam fc  umeandaa mashindano yajulikanayo kama Azam Youth Cup kwa vijana wa umri wa chini ya miaka 20 huku wakiwaalika  nchi za Kenya, Uganda na Mauritius yatakayofanyika kuanzia Juni 2 katika viwanja vya Azam Complex.

Dhumuni la kuandaa mashindano hayo, ni kuwaandaa vijana wa baadae watakaoleta soka la ushindani kwani nchi hususani katika ligi pamoja na timu ya Taifa. Akisema hayo mtendaji mkuu wa Azam, Saady Kawemba amesema mashindano hayo yatakuwa ni endelevu kwani  mpango wao ni wa miaka 12 kuanzia 2016 na kila mwaka watakuwa wanaalika timu tofauti tofauti.

"Huu ndo mwaka wa kwanza tumeanza kuandaa mashindano haya ya vijana na mpango wetu ni wa miaka 12 mbela kwahiyo tunaanza na nchi tatu tumezialika kutoka Kenya, Uganda na Mauritius ila kila mwaka tumeazimia kualika nchi tofauti kwani lengo kuu ni kuona vijana wanaonyesha uwezo wao ikiwemo kuja kuchezea timu zao za Taifa,"amesema Kawemba. 

Amesema kuwa timu zinatarajiwa kuingia Mei 30 na siku inayofuata kutakuwa na semina kwa washiriki wa mashindano hayo na Juni 02 yataanza rasmi kwa mechi mbili kuchezwa kila siku asubuhi na jioni, mshindi wa mashindano hayo atapatikana kwa kuwa na alama nyingi katika michezo atakayokuwa amecheza. Mbali na hilo Kawemba ameweka wazi mkakati wa klabu ya Azam katika kuwekeza kwenye soka la vijana kwani kwa sasa wameandaa timu zingine mbili tofauti na ile ya Vijana inayoshiriki katika mechi za ligu kuu.

Amesema, lengo kuu la Azam ni kuja kuona kuwa soka la Tanzania linafika mbali hususani kwa vijana wachanga wanaochipukia ikiwemo kupata nafasi za kucheza nje ya nchi  na kuiwakilisha vyema taifa na kuwa kama nembo.
Wakati huo huo.
AZAM WAMTAKIA MAISHA MEMA KINDA FARID MUSSA, TENNERRIFE.
MTENDAJI mkuu wa Azam Fc, Saady Kawemba amesema kuwa Farid Mussa (Pichani)ana baraka zote kutoka kwao katika maisha yake mapya ya soka nchini Hispania kwenye timu ya Tennerrife kwa mkataba ambao utakuwa na manufaa kwake na klabu pia kwani watapata nafasi nzuri ya kupeleka vijana wengine kwenye timu za nchini Hispania.

Kawemba amesema watatumia nafasi hiyo kuweza kupeleka vijana wengine ikiwa ni lengo la kutanua wigo wa wachezaji wa kitanzania kwenye soka nje ya nchi hususani nchi za ulaya.

Farid amepata nafasi ya kujiunga na timu hiyo huku wakitumia mechi yao dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa fainali ya FA kumuaga pamoja na kumpa baraka zote. Kawemba amesema kwa sasa Farid hayupo kwenye mpango wa mwalimu kuanzia mechi ya Yanga na msimu unaokuja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...