TIB imefanya mabadiliko ya kitaasisi ili kuweza kuwa kituo cha huduma zote za kifedha kwa kushughulikia mahitaji ya wawekezaji wa ndani wote kwa lengo la kusukuma maendeleo ya uchumi wa taifa.Mwanza, 5, May-2016: Benki ya Rasilimali nchini (TIB) imesema imekusudia kuwawezesha kifedha wakandarasi wa ndani ili waweze kutekeleza vema majukumu yao ya ujenzi wa miradi ya barabara na mingineyo.

Akizungumza wakati wa mkutano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi nchini (CRB) uliofanyika jijini Mwanza, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo ya Mikopo wa Benki ya TIB, Theresia Soka amesema mikopo inayotolewa na benki yake kw wakandarasi wazawa nchini haihitaji mhusika kuweka dhamana benki. 

‘Benki ya Rasilimali imemua kurahisisha taratibu zake za kutoa mikopo kwa wakandarasi wa ndani, na tunachohitaji kwa mkandarasi anayetaka tumpe mkopo wa fedha atuletee vielelezo tu vinavyomtambulisha kuwa yeye ni mkandarasi na amesajiliwa kisheria’ alisema Bi Soka. 

‘Tumeamua kuwawezesha wakandarasi kwa lengo la kusaidia ukuaji wa maendeleo nchini katika sekta hii muhimu ya ujenzi’ alisema Bi Soka. Naye Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa TIB, Bahati Minja, alisema benki hiyo inayomilikiwa na Serikali, imeboresha huduma zake za kibenki ndiyo maana inahitaji kuwawezesha wakandarasi wazawa nchini. 

‘Lengo kubwa la Benki ya TIB ni kuhakikisha wakandarasi tunawawezesha kifedha ili wawe na vitendeakazi, yakiwamo magreda’ alisema Bi Soka. Minja aliwaomba wadau hao wa maendeleo kuchangamkia fursa hiyo kwa kuchukuwa mikopo itakayowasaidia katika majukumu yao. 

Hata hivyo makandarasi waliohudhuria mkutano huo ambao miongoni mwa wafadhili wake ni benki hiyo, waliupongeza uongozi wa Benki ya TIB kwa kuamua kuwawezesha mikopo wakandarasi. Wakandarasi hao walisema uwezeshwaji huo wa mikopo nafuu inayotolewa na benki hiyo, itawasaidia kuendesha kampuni zao za ujenzi. 

Mkutano huo utafuatiwa na mkutano mwingine utakaofanyika jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Daimond Jubilee kuanzia tarehe 26 hadi 27 mwezi huu wa tano, mwaka huu una kauli mbiu ya ‘Kuwajengea Uwezo Wakandarasi wa Ndani kwa ajili ya Uchumi Endelevu: Changamoto na Mipango ya baadae’. 

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Benki ya Rasilimali nchini (TIB), Bahati Minja (aliyesimama) akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa mkandarasi mkoani Mwanza, kuhusu huduma bora za mikopo zinazotolewa na TIB kwa wakandarasi nchini katika mkutano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi nchini (CRB) uliofanyika jijini Mwanza jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...