Shindano la Mama Shujaa wa Chakula msimu wa tano limeingia katika hatua ya pili ya kupokea fomu na kuwachuja wakina mama waliotuma maombi ya ushiriki wao baada ya hatua ya mwanzo ya kugawa fomu hizo kufanyika katika uzinduzi wa shindano hilo mkoani Mtwara mapema mwaka huu.

Fomu hizo zimepokelewa leo katika kituo cha mazoezi cha Azura jijini Dar ambapo timu ya majaji kumi kutoka taasisi mbalimbali walizipitia fomu hizo katika zoezi litakalochukua takribani wiki nzima hadi kukamilika kwake.

Kwa mujibu wa Afisa Miradi kutoka shirika la kimataifa la Oxfam, Kefah John, alisema kuwa takribani washiriki 3,000 wametuma maombi yao kupitia fomu hizo ambapo katika hatua ya kwanza watapatikana washiriki 28 ambao watachujwa na kubakia washiriki 18 watakaopiga kambi mkoani Monduli, Arusha na hatimaye kumpata mshindi mmoja.

Wakizungumza na waandishi wa habari, msanii Jacob Stephen JB na mtangazaji wa EFM, Dina Marios ambao ni mabalozi wa shindano hilo, waliwahamasisha wakina mama watumie shindano hilo litakalorushwa laivu kupitia kituo cha televisheni ya ITV ili kujifunza njia mbalimbali za kuboresha uzalishaji wao ili kukuza kipato cha familia.

Meneja Utetezi wa Shirika la kimataifa la OXFAM, Eluka Kibona akizungumza neno la utangulizi wakati wa hafla ya maamuzi ya Fomu za Mama Shujaa wa Chakula shindano linaloendeshwa na Shirika la Kimataifa la OXFAM kwa mwaka 2016.
Afisa Miradi kutoka Shirika la kimataifa la OXFAM Kefah Mbogela akizungumzia juu ya Shindano la Mama Shujaa wa Chakula, Umiliki wa Ardhi na Changamoto za ardhi na mitaji ili kujiendeleza.
Katikati ni aliyekuwa mshiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa chakula 2014, Ester Kulwa akiwahamasisha wakina mama kushiriki katika Shindano la Mama Shujaa linaloendeshwa na Shirika la Mataifa la OXFAM.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...