Mkuu wa Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Kamishna Msaidizi Juma Yange akitoa maelezo namna kisima cha maji maalumu ya Zimamoto (fire hydrant) kinavyofanya kazi kwa Kamishna Jenerali Thobias ndengenye alipotembelea kituo hicho mapema leo.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye akijitambulisha kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Ramadhani Maleta alipotembelea leo uwanja huo wakati akiwa kwenye muendelezo wa ziara yake ya kutembelea vituo vya zimamoto na uokoaji nchini.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye akitoka kukagua ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linalojengwa eneo la Tazara Mchicha mapema leo asubuhi alipokuwa akiendelea na ziara yake ya kutembelea vituo vya Zimamoto katika Jiji la Dar es salaam. (Picha na FC Godfrey Peter)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 05, 2016

    Serikali iangalie uwezekano wa kuwekeza zaidi katika idara hii nyeti kwa kuwapatia vitendea kazi bora.imekuwa kawaida yetu kuto on a umuhimu wa idara hii mpaka pale majanga ya moto yanapotokea.
    Na ili kuofanya idara hii kuwa more relevant serikali ingeanzisha kitengo cha paramedics (ambulance service )ndani ya idara hii.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 06, 2016

    Nimefurahishwa na Uteuzi wa Kamanda Andengenye,nina imani kuwa nanakuja kufanya mageuzi makubwa sana kwenye idara hii nyeti!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...