Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KOCHA  wa Simba, Mganda Jackson Mayanja amesifia kiwango kilichooneshwa na wachezaji wake kutoka kikosi B na kuweza kucheza kwa kujituma zaidi ingawa wamepoteza mchezo huo kwa jumla ya goli 2-1 na kuweza kusalia kwenye nafasi ya 3 ya msimamo wa ligi.

 Simba imejitahidi  kupambana kuweza kuchukua ubingwa msimu huu lakini juhudi hizo zimegonga mwamba baada ya watani wao kutetea ubingwa huo kwa mara mbili mfululizo.  Kocha Mayanja amesema kuwa ni mara chache ndani ya timu  kuona vijana wa timu B wanapewa nafasi katika mechi za ligi kuu kwan ameona vijana hao katika mazoezi kabla hata ya mchezo wao dhihi ya timu ya Majimaji ya mjini Songea.

"Nimevutiwa na uwezo wa vijana hawa kabla hata ya kwenda Songea katika mchezo dhidi ya Majimaji na uwezo wao ndio uliofanya niwapange tena dhidi ya JKT Ruvu" amesema Mayanja. Akizungumzia mchezo wao wa mwisho wa ligi Mayanja amesema kuwa kikosi chake hakikucheza vizuri jambo lililopelekea kupoteza mchezo huo.

Amesema endapo wachezaji wangekuwa makini wangeshinda mchezo huo kutokana na kupoteza nafasi nyingi walizozipata hasa katika kipindi cha kwanza. "Kikosi changu hakikucheza vizuri katika mchezo wa leo kwani wamepoteza nafasi nyingi walizozipata", amesema Mayanja.

Katika michezo 20 ya kocha huyo toka aanze kuinoa Simba amefanikiwa kushinda michezo 12, droo nne na kupoteza minne.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...