Msanii Wa Bongo Fleva Snura Mushi (Snura) amewaomba radhi watanzania kwaujumla pamoja na vyombo vya serikali vinavyosimamia sekta ya sanaa kwa kutokufuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo katika uendeshaji wa sanaa.

Ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, radhi hiyo imekuja mara baada ya Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo jana kufungia video ya wimbo wa msanii huyo wa Chura ikiwa ni pamoja na kutoonyeshwa kwenye Televisheni pamoja na kupigwa kwenye redio. Amesema kuwa tayari  video ya wimbo huo ameshatoa kwenye mtandao wa kijamii wa Youtube.
Msanii Wa Bongo Fleva, Snura Mushi (Snura) awaomba radhi watanzania kwa kufanya video isiyo na maadili ya kitanzania ya wimbo wake wa Chura ameomba radhi watanzania mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Meneja wa msanii Wa Bongo Fleva, Snura Mushi (Snura), Hemed Kavu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo na kuwaomba radhi wa tanzania kwa video ya wimbo wa Msanii Snura na wimbo wake wa Chura.

Kulia ni Msanii Wa Bongo Fleva, Snura Mushi (Snura) na Kushoto ni meneja wa msanii huyo, Hemed Kavu.
Snura amesema kuwa yupo tayari kufanya upya video ya Wimbo wake wa chura ambayo itafuata maadili ya kitanzania kwani tayari ameshachukua vibali vya kufanya upya video ya wimbo huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 05, 2016

    Hivi huyu mdada wazazi wake wote wapo hai kweli??? hiyo video anaweza kukaa yeye, kaka yake na wazazi wake wote wawili wakaiangalia kweli??? Wasani kuweni na busara

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 05, 2016

    Snura thumbs Up baby, just express your opinion, its all Arts, never give up to draconian laws
    Alex bura Dar

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 06, 2016

    Mimi nimeisha sema siku nyingi huyo dada sio mzima na hata maneja wake pia, naye sio mzima.nakuomba weke hiyo video yako na familia yako, harafu uniambie watakuambia nini? Unafanya vitu kama vile Tanzania sio kwenu. Nenda ukakae ndani ya maji na hiyo michezo yako ya chura , harafu uone chura na samaki watakufanya nini

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 06, 2016

    Maadili ni zero + zero = zero. Mungu anasubiri tu wakati ufike ili kila mwanadamu atoe HESABU kwamba alielimisha jamii kwa kiwango gani ili kumcha Mola ama alichangia vipi kuifanya jamii KUANGAMIA. Huyu dada hana maadili hata ya kidini.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 06, 2016

    Huyu msanii sijui alijikuza mwenyewe na hana wadogo waka wakubwa kwao wa kuwaheshimu?? Hivi kweli video kama ile anaona inafaa kabisa kuangaliwa na wakubwa na wadogo? Kweli Wasanii sasa hivi wanapokwenda sipo kabisaa... Maadili yamevunjika kabisa..

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 06, 2016

    Tatizo ni nini? Video iko bomba, thumb up Snura

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...