Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
 KWA mujibu wa mtandao wa Goal.com kinda wa Yanga na winga machachari Geofrey Mwashiuya ametabiriwa makubwa sana kutokana na uwezo wake anaouonyesha kwenye mechi za timu yake ikiwemo mchezo wa kimataifa dhidi ya GD Esperanca.

Mwashiuya ambaye amesajiliwa na Yanga msimu huu unaomalizika akitokea timu ya Kimondo inayoshiriki ligi daraja la kwanza, nalll kuweza kuonesha uwezo wa hali ya juu kilichopelekea kuwa wa nyota wa kutumainiwa katika kikosi hicho kwa kuweza kuisaidia kweny bb mbalimbali ikiwemo dhidi ya Simba akitoa pasi ya goli la pili na kufungwa na Amisi Tambwe.

Kwenye mchezo wa kwanza wa hatua  ya 16 bora ya kombe la Shirikisho Afrika, Mwashiuya alionekana ni mwiba kwenye lango la upinzani na kutoa pasi ya mwisho ya goli lililofungwa na Simon Msuva.

"Nina imani kuwa kama mwalimu ataendelea kunipanga mara kwa mara nitazidi kuonyesha uwezo wangu na nitajituma zaidi kuweza kufikia malengo yangu ya kucheza soka la kulipwa nje kwani kila kitu ni kumuamini mungu,"amesema Mwashiuya.

Mwashiuya amekuwa ni moja kati ya vijana 10 waliotabiriwa kufanya vizuri  huku yeye akiwa na umri wa miaka 19 akiwa anaiwakilisha timu yake ya Yanga kwenye michuano ya kimataifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...