Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi amesimamishwa kuhudhuria vikao kumi vya bunge kuanzia leo June 30 mwaka huu baada ya kubainika kunyosha kidole cha kati kwa wabunge baada ya kukiri mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka kwamba alifanya kitendo hicho. Hata baada ya kuhojiwa Mbunge Mbilinyi alishindwa kumtaja Mbunge wa CCM aliyedaiwa kumtukana ili nae achukuliwe hatua na kamati hiyo. Bunge limeridhia adhabu hiyo iliyotolewa na kamati.
Mbunge wa Ubungo Chadema Saed Kubenea amesimamishwa kuhudhuria vikao vitano vya bunge na Naibu Spika Dk Tulia Akson baada ya kubainika kusema uongo kwamba Waziri wa Ulinzi na JKT Dk Hussein Mwinyi ameingia Mkataba na kampuni ya China Henan International Cooperation Group Company wa ujenzi wa nyumba za JWTZ na nyumba ya Waziri huyo jambo ambalo sio kweli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 30, 2016

    Hapa tatizo lipo kwenye hiyo mipesa wanayo lipwa ni mipesa mingi sana ndio maana wanafikia kusema chochote coz pesa zimewalevya sasa sijui ndicho walichotumwa na wapiga kura wao? majimboni kwao kuna shida lukuki lakini chaajabu hawazisemei minaona sasa niwakati muufaka wa kuwa na mahakama ya bunge ili wanaokiuka sheria za bunge wahukumiwe huko huko na ikiwezekana wafungwe pia

    ReplyDelete
  2. MBUNGE NI MWAKILISHI..NA UWAKILISHI MAANA YAKE UKASEME ULIYOPOKEKEA TOKA KWA ALIYEKUTUMA...SASA UMAANA HUO UMETUPWA NA BADALA YAKE MBUNGE ANAJIWAKILISHA MWENYEWE HAYO NDO MATOKEO YAKE ACHA MUNGU ����AWAKUMBUSHE ANGALAU KWA ADHABU HIZO NDOGONDOGO!!!Na mmd

    ReplyDelete
  3. MUNGU NAYE AMEWAONE ...NA HILO NI ONYO KWAO KWA KUKIUKA YALE WALIYOTUMWA ...WAMESAHAU KUWA WAO NI WAWAKILISHI TU.(Na mmd!!)

    ReplyDelete
  4. MUNGU NAYE AMEWAONE ...NA HILO NI ONYO KWAO KWA KUKIUKA YALE WALIYOTUMWA ...WAMESAHAU KUWA WAO NI WAWAKILISHI TU.(Na mmd!!)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...