HAIKUWA hali ya kawaida ila ukihadithiwa ni kama hadithi za sungura na fisi ila umati wa maelfu ya Watanzania ilistaajabisha umma na kila mmoja kujiuliza hivi kweli zaidi ya watu elfu hamsini (50,000) waliojitokeza Uwanja wa Taifa kuishuhudia mechi kati ya Yanga na TP Mazembe, hawakuwa na shughuli za kufanya? Achilia kuajiriwa ila hata kujiajiri pia? 
Hilo ni swali la kujiuliza kwani majira ya saa 12 asubuhi (Jumanne, siku ya kazi) watu walikuwa wameshafurika kwenye mageti yote ya kuingia Uwanja wa Taifa kwa ajili ya kushuhudia mechi hiyo ambayo changamoto mbalimbali ziliweza kuonekana ikiwemo utaratibu wa kuingia kuwa mgumu hasa baada ya uwanja kujaa. Uwanja wa Taifa unachukua watu zaidi ya elfu hamsini (50,000) na kwa hali ilivyoonekana jana kama ungeingia watu zaidi ya idadi halisi, labda pengine hata mchezo wenyewe usingeweza kuchezwa, kwani wangeingia mpaka kwenye dimba la kati unakochezewa mchezo huo.
 Je, kujitokeza kule kwa wale watu kunatokana na nini, Je ni kwamba hawakuwa na shughuli za kufanya, na kama wanazo walimuachia nani na kwa nini? na kama ni mapenzi ya Mchezo wa Soka waliyonayo ndio imepeleka kujitokeza kwa wingi wa namna Ile na ndio kuanzia asubuhi yote ile wakati mechi ilichezwa saa kumi (10:00) jioni??  Tunadhani kuna haja ya kujiuliza sana juu ya swala hili, maana kwa siku ya Jumanne tena mwanzoni mwa wiki watu wengi kujitokeza namna ile ni jambo la kushtua kidogo. 
Ruksa kujadili mradi usichafue hali ya hewa....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. this event has a lot of definitions n i think some reasons ar there is no employment; n sometimes to a fun of a certain team is the same to a slave in tbat mantic but govt now should take thoroughly measures after this situation to happen yesterday we ar waiting for a job majority who ar coming from very poor family n theres no capital which can make us survive in terms of working bro michuzi we graduates n there's no hob wat else do u think these guys as tzns will do rather than b a jobless n waiting for an opportunities like that. Submission please.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 30, 2016

    Watu wetu wanapenda mno kuporoja.
    Hivi kuna nchi gani yenye umaskini unaoshabihiana na Tanzania ambako hakuna tatizo la ajira?
    Hapa UK pamoja na maendeleo ya juu yaliyofikiwa, bado ajira haijapatiwa ufumbuzi. Na US na kwingineko kwingi. Sasa kwa nini basi tuufumbie macho ukweli?
    Bora mtu kama hana la maana la kusema na anyamaze. Tanzania ina maelfu ya mbinu za kujipatia riziki na si leo wala kesho ajira ya kiwandani wala ofisini haitatosheleza. Tuache ukasuku na tuishi ndani ya ukweli.
    Vijana hawataki kujishughulisha badala yake wanaendekeza uzururaji na chilling out. Na kwa masikitiko kuna wenzetu wanawahalalishia uzembe huo.
    Ni msiba kwa Taifa letu changa.
    Mndengereko Ukerewe

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 30, 2016

    Kama kiingereza cha 'graduate' ndo hichi nani akupe kazi? Anko Michuzi kwa nn unapublish upupu kama huo kwenye uwanja huu WA jamii? Tarime

    ReplyDelete
  4. fred mutahJune 30, 2016

    KILA KITU KIPO WAZI KUNA TATIZO TENA KUBWA SANA..SINA UHAKIAKA SANA NA MIPANGO YA KUPATIA VIJANA AJIRA ILA LA MSINGI NI KUWA WEWE NA MIMI TUMEJIPANGA VIPI KWA AJILI YA WATOTO WETU...TUNAPANGA UZAZI KWELI?

    KWA UPANDE WAS SERIKALI INAPASWA SASA KUWEKA NGUVU SANA MIKOAN ILI VIJANA WENGI WABAKI HUKO...FURSA ZIPO NYINGI SANA MIKOAN KULIKO DAR ES SALAAM ILA DAR KUNA MZUNGUKO MKUBWA WA PESA.

    TUNATEGEMEA KWA MFANO KUFUTA MATUMIZI YA MIFUKO WA PLASTIC KULINGANA NA WAZIRI WA MAZINGIRA...JE KUNA KUKUNDI CHOCHOTE KINA PLAN YA KUTENGENEZA VIKAPU...MIFUKO YA KARATAS NA VITAMBAA? FURSA YA WAZI HII KABISA KAMA KIPO KIWEZESHWE NI KWA FAIDA YA MAZINGIRA NA WATU PIA.

    JE WIZARA YA KAZI HAIWEZI KUWEZESHA VIJANA KWA HILI? ...

    ASUBUHI NJEMA

    ReplyDelete
  5. Umati haukusababishwa na ukosefu wa ajira mbona mnataka kupindisha ukweli wakati kila kitu kipo wazi!! Wale watu asilimia 80 kila mtu ana kibarua chake cha kumuingizia riziki. Kilichosababisha umati ni mambo mawili yaliyotokana na ja jambo moja. Kitendo cha Yanga (uongozi) kutangaza mechi itakuwa bure ndo kimejaza umati, lkn pia MKAKATI wa yanga kutamani 'SIMBA' wakose nafasi ya kuingia uwanjani hapo kwa wingi kuishangilia MAZEMBE uliwalazimu mashabiki wake kujitokeza tangu alfajiri na kuketi sehemu kubwa ya uwanja ili wale wa simba wakija saa 6 mchana wakute nafasi chache au ikiwezekana wakose nafasi kabisa..wao waliamini simba wangeishangilia MAZEMBE ingeshinda. KUMBUKA ilikuja mpaka timu ya taifa ya BRAZIL na uwanja haukujaa saa 5 asbh,kadhalika simba ilipocheza na MAZEMBE miaka michache nyuma, sahau kuhusu mechi zingine za simba na waarabu au yanga yenyewe na waarabu! BURE GHALI + SIASA ZA MAJITAKA ZA VIONGOZI WA SOKA TZ-KUKOMOANA
    Asante!

    ReplyDelete
  6. Huenda tumekua too judgmental, na wala sio tatizo la Tanzania kwamba watu hawafanyi kai kwa tukio la siku moja, kwanza ikumbukwe ile mechi ilikua BURE, Halafu ni mechi kubwa sana yenye tension hivyo kulazimu watu kuua siku nzima, huenda kuna ukweli kwamba walio wengi ni ambao hawana ajira lakini hatuwezi kufanya inductive reasoning ju justify ...mahaba ya mpira ni kitu kingine kabisa...............pili naona kabisa mfumo wa viwanja vyetu bado ni wa kishamba ati watu wanaingia kwa kugombea viti inaglikua kila mtu anaingia kwa namba ya kiti chake haya yasingelitokea tena watu wanahesabiwa kwa mashine badala ya kuhesabu kwa macho au vidole cum tallying

    kuhus Yanga kuamua BURE ni matokeo ya malumbano ambayo hayana tija kwa Taifa zaidi ya watu kuwa emotional than rational tushukuru sana hakukua na majnaga makubwa maana ingalikua ni habari nyengine kabisa

    TFF ichukue mandate yake badala ya kuburuzwa na wenye PESA maana ule ni uwanja wa TAIFA sio wa Kaunda

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 30, 2016

    Naunga mkono hoja ya mndengereko, sisi si nchi ya kijamaa tena. Tuko kwenye mfumo wa kibepari tangu enzi za Mwinyi. Maana yake kila mtu jukumu la kujikidhi yeye binafsi pamoja na familia yake. Ndo maana nchi zilizoendelea walioanzisha huo mfumo hawazai watoto wengi kama hawawezi kuwategemea na hawalaumu serikali zao kukosa ajira. Serikali kazi yake ni kukusanya kodi na kuitumia kukupatia huduma muhimu kama usalama, miundombinu,n.k. Sio kukutafutia kazi au soko. Ubepari ni baba ya soko huria. Ubeparini asiyefanya kazi hali hata kama Ana mjomba au kaka. Kwahiyo wanasiasa wajinga wajinga ndo wanapotosha hao vijana na kuwapotosha,bila kuwaeleza kuwa kupiga siasa ndo kazi yao inayowaweka mjini hata kama ni zakupotosha. Nasali hawa vijana waamke wajielewe, laasivyo wataendelea kutumika na kufa masikini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...