Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi akipokea Ripoti ya Tamasha la Michezo ya Shirikisho la Vyuo Vikuu, kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho hilo, Abdullatif Kadir Mussa iliyomalizika mapema mwezi huu. Kushoto ya Balozi Seif ni Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la Shirikisho hilo ambae pia ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Zanzibar Mh. Ayoub Mohammed Mahmoud, Mkuu wa Wilaya ya Kusini Nd. Idrissa Kitwana na Katibu Mkuu wa Zahilfe Nd. Juma Omar Ali.
Balozi Seif akiuahidi Uongozi wa Zahilfe kuunga mkono katika kufanikisha malengo yao ya Shirikisho hilo la Vyuo Vikuu na Taasisi ya Elimu ya Juu Zanzibar.
Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la Shirikisho la Vyuo Vikuu na Taasisi ya Elimu ya Juu Zanzibar Mh. Ayoub Mohammed Mahmoud akimpongeza Balozi Seif kwa kusaidia kufanikisha Tamasha la Shirikisho hilo. Picha na – OMPR –ZNZ.

Uongozi wa Shirikisho la Vyuo Vikuu na Taasisi ya Elimu ya Juu Zanzibar {ZAHILFE }umepata mualiko wa kushiriki kwenye Mkutano wa Kimataifa wa masuala ya Amani ya Dunia unaotarajiwa kufanyika Nchini Benin iliyoko Magharibi mwa Bara la Afrika.

Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo Ndugu Juma Omar Ali akiuongoza ujumbe wa Viongozi wa Shirikisho hilo  alieleza hayo wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ripoti ya Tamasha la Michezo ya Shirikisho hilo iliyomalizika mapema mwezi huu.

Nd. Juma Omar alisema ushiriki wa Viongozi hao katika Mkutano huo wa Kimataifa utaoanza Tarehe 24 hadi 27 Mwezi Agosti mwaka huu utafungua njia kwa wanachama wa shirikisho hilo kupata uzoefu kupitia taasisi nyengine za Elimu ya juu Duniani.

Alisema mpango wa baadaye wa Shirikisho hilo katika kujiimarisha kiajira sambamba na kusaidia Vijana wanaomaliza masomo yao umelenga kutafuta fursa za Taaluma katika sekta ya Uvuvi ili iwafungulie njia ya kuanzisha vikundi vya ujasiri amali.

Alisema Visiwa vya Zanzibar vimebarikiwa kuzunguukwa na Rasilmali ya Bahari ambayo kwa karne nyingi zilizopita bado haijutumiwa ipasavyo tokea kuumbwa kweka ambayo inaweza kutoa mchango wa ajira kwa kundi kubwa la vijana sambamba na kuongeza mapato ya Taifa.

Akizungumzia Tamasha la mwaka huu la Michezo ya Shirikisho hilo la Vyuo Vikuu na Taasisi ya Elimu ya Juu Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo Nd. Juma alieleza kwamba michezo hiyo ilikuwa ya aina yake kiasi kwamba washiriki wake waliweza kutoa burdani safi iliyoshamiri ndani ya Mji wa Zanzibar.

Alifahamisha kwamba maandalizi ya Timu za Zanzibar kwa ajili ya mashindano ya Kitaifa ya Vyuo Vikuu na Elimu ya Juu Tanzania nay ale ya Kimataifa yameanza rasmi ili kuwapa muda mrefu zaidi Vijana hao wa kufanya vyema kwenye kinyang’anyiro kinachowakabili.

Nd. Juma alielezea furaha yake kutokana na Uongozi wa Mashindano ya Kitaifa   Tanzania kuiamulia Zanzibar kupeleka Timu Nne za Mpira wa Soka na Timu 3 za Mpira wa wavu kwenye  Mashindano hayo ya Taifa ya Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania.

Akipokea Ripoti hiyo ya Tamasha la Michezo ya Shirikisho la Vyuo Vikuu na Elimu ya Juu Zanzibar { ZAHILFE } Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali itaunga mkono shirikisho hilo kutokana na nia yao nzuri ya kuanza na michezo na baadaye nguvu zao kuzielekeza katika uchumi.

Balozi Seif aliuhakikishia Uongozi wa Shirikisho hilo kwamba atafanya juhudi za ziara wakati atapokutana na Uongozi wa Balozi wa China Nchini Tanzania kuomba fursa za masomo ya fani ya Uvuvi kwa vijana hao kwa lengo la kuunga mkono mawazo yao ya kutumia fursa za ajira katika sekta hiyo.

Alisema ziara za mafunzo ya uvuvi ndani na nje ya nchi ni muhimu kwa vile yatafungua milango ya fursa za ajira kwa kundi kubwa la wasomi wanaomaliza masomo yao ya sekondari badala ya kukaa wakisubiri ajira za Serikali ambazo ni finyu kwa wakati huu.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliushauri Uongozi wa Shirikisho hilo la Vyuo Vikuu na Taasisi ya Elimu ya Juu Zanzibar { ZAHLIFE } kuendeleza michezo kwa vile inaleta upendo, urafiki, mshikamano na hata ajira kwa Vijana.

Mapema Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la Shirikisho la Vyuo Vikuu na Taasisi ya Elimu ya Juu Zanzibar ambae pia ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohammed Mahmoud alimpongeza Balozi Seif licha ya kuwa mgeni katika ufungaji wa Tamasha hilo lakini pia alisaidia kuona Tamasha hilo linaanza na kumalizika kwa mafanikio.

Mh. Ayoub alisema mchango wa Balozi Seifm kwa Shirikisho hilo umekuwa Dira na matumaini mapana kwa wana Shirkisho hilo katika hatua ya mtyazamo wa baadaye wa Taasisi hiyo iliyokusanya wasomi wa elimu ya Juu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...