Kikosi kazi cha Mfuko wa Pensheni wa LAPF inayoshiriki  maonyesho ya biashara ya kimataifa (Saba Saba) ikiwa ndani ya banda nadhifu ambapo huduma mbalimbali zinatolewa kwa wanachama na wadau mbalimbali wa Mfuko.

 Banda la Mfuko wa Pensheni wa LAPF likionekana kwa nje likiwa na unadhifu wa hali ya juu, mbele ya banda ni timu ya maofisa wa LAPF wakiwa tayari kuhudumia wageni wote wanaofika katika banda la Mfuko kwenye maonyesho ya biashara ya kimataifa 2016.
Maafisa wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya banda nadhifu la Mfuko huo katika maonyesho ya biashara ya kimataifa 2016.
 Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. James Mlowe akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sababu za ushiriki wa Mfuko katika maonyesho ya biashara ya kimataifa (Saba Saba 2016).
Afisa Mifumo ya kompyuta kutoka Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. Yohana Nyabili akitoa maelezo kwa mwanachama wa Mfuko pamoja na kumpatia taarifa ya michango yake mara baada ya mwanachama huyo kutembelea banda ya Mfuko kwenye maonyesho ya biashara ya kimataifa (Saba Saba 2016).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...